WATUMISHI wa afya 21 kutoka kitengo cha kuhudumia watu waliopatwa na majeraha katika ajali  (trauma unit) cha Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo kutoka kwa wataalam wa matibabu kutoka Israeli. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dr Alphonse Chandika, amebainisha kuwa mafunzo hayo ya siku sita yaliandaliwa kwa ajili ya kuwapatia maarifa wataalamu…

Afisa muuguzi msaidizi wa Idara ya Uuguzi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Ndg, Elias Kibiki, ameibuka kuwa mfanyakazi bora wa mwaka wa BMH katika siku ya wafanyakazi, Mei Mosi. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk, Binilith Mahenge, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika sikukuu hiyo amemkabidhi Ndg, Kibiki cheti na hundi yenye thamani ya…

Watu wapatao 3,500 wamefanyiwa uchunguzi wa macho bure kupitia mpango maalumu unaoneshwa na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) katika maeneo ya vijiji ya mkoa wa Dodoma. Hii ilibainishwa siku za karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dr Alphonce Chandika, akielezea watu wapatao 500 waliopatikana na matatizo ya macho walifanyiwa upasuaji katika zoezi la miezi miwili….

IKIWA na vifaa vya matibabu vya kisasa, Hospitali ya Benjamin Mkapa (BHM) inapanga kuwa kitovu cha utalii wa matibabu cha nchi baada ya kuanza kutumia ofisi za ubalozi za nchi kujitangaza juu ya huduma bora inazotoa. Utalii wa matibabu (medical tourism) ni pale watu wa nchi moja wanaposafiri kwenda nchi ingine kupata huduma za matibabu….

Copyright © 2020 - Benjamin Mkapa Hospital All rights reserved

Privacy Policy    |   Disclaimer   |    Sitemap   

English English Swahili Swahili