choose language English English Swahili Swahili

Afisa muuguzi msaidizi wa Idara ya Uuguzi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Ndg, Elias Kibiki, ameibuka kuwa mfanyakazi bora wa mwaka wa BMH katika siku ya wafanyakazi, Mei Mosi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk, Binilith Mahenge, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika sikukuu hiyo amemkabidhi Ndg, Kibiki cheti na hundi yenye thamani ya 1m/- kwa ajili ya kutambua mchango wake kwa BMH.

Ndg, Kibiki ameelezea furaha yake kwa kuchaguliwa kwa kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora wa Hospitali hiyo ya umma, akisema tuzo hiyo imempa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii katika.

“Nawashukuru wafanyakazi wenzangu kwa kuona utendaji wangu na kunichagua kuwa mfanyakazi bora,” alisema baada ya kukabidhiwa zawadi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Ndg, Kibiki  ameuomba uongozi wa BMH kuangalia uwezekano wa kila kitengo katika hospitali hiyo kuwa na mfanyakazi bora katika sikukuu zijazo za Mei Mosi.

“Hii itaongeza hamasa zaidi kwa wafanyakazi wa kila kitengo hapa hospitalini hvyo kuzidi kuboresha ufanisi wa shughuli,” alihitimisha.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, (kushoto) akimkabidhi cheti na hundi yenye thamani ya 1m/- mfanyakazi bora wa mwaka wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Afisa Muuguzi Msaidizi, Ndg. Elias Kibiki wakati wa sikukuu ya wafanyakazi (Mei Mosi).

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano cha BMH

CategoryNews

Copyright © 2020 - Benjamin Mkapa Hospital All rights reserved

Privacy Policy    |   Disclaimer   |    Sitemap   

English English Swahili Swahili