choose language English English Swahili Swahili

Waandishi wa Habari Watembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa

WAANDISHI wa habari wapatao 30 kutoka vyombo mbalimbali vya habari wametembelea
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kujionea uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kupitia
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Meneja Mawasiliano wa NHIF, Angela Mziray, anasema ziara hiyo iliyoratibiwa kwa pamoja na
Klabu ya Waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma (CPC) ililenga kuonesha faida za kujiunga
na NHIF.


“Ziara hii itawasaidia waandishi wa habari kuelimisha umma juu ya faida za kujiunga na NHIF,”
alisema Meneja Mawasiliano wa NHIF wakati wa kuhitimisha ziara hiyo ya waandishi wa habari.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa BMH, Karimu Meshack, alisema kuwa BMH
imeisaidia serikali kuokoa fedha nyingi ambazo zingezitumika kwa ajili ya kupeleka wananchi nje
ya nchi kwa ajili ya matibabu.
“BMH tumeshapandikiza figo kwa wagonjwa saba mpaka sasa. Hivyo tumesaidia kupunguza
rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi,” alisema bwa, Meshack.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya figo wa Hospitali hiyo, Dk, Kessy Shija,
alisema kumekuwa na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza kutokana na mabadiliko ya
mtindo wa maisha miongoni mwa watu.
Dk, Shija alisema kuwa NHIF imesaidia kugharimia matibabu ya wanachama wa mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya na kutolea mfano kwamba matibabu kwa wagonjwa wa figo yanafikia milioni
mbili kwa mwezi.

Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano,
BMH

CategoryNews

Copyright © 2020 - Benjamin Mkapa Hospital All rights reserved

Privacy Policy    |   Disclaimer   |    Sitemap   

English English Swahili Swahili