PEOPLE who have obesity in the country can now breathe a sigh of relief after the Benjamin Mkapa Hospital (BMH) to start performing bariatric surgery, an operation performed on people who have obesity.

Bariatric surgery or weight loss surgery is achieved by reducing the size of the stomach with a gastric band or through removal of a portion of the stomach (sleeve gastrectomy or billiopancreatic diversion with duodenal switch or resecting and re-routing the small intestine to a small stomach pouch (gastric bypass surgery).

Executive Director of the Benjamin Mkapa Hospital, Dr Alphonse Chandika, noted here yesterday that the public Hospital has already successfully performed the bariatric operation on one person with obesity.

“We have successfully performed bariatric surgery on one young person with obesity yesterday,” said the Hospital’s Executive Director while briefing on laparoscopic camp at the BMH.

BMH, a four hundred bed health facility, is conducting a laparoscopic camp which ends today. At least 500 people who hail from Mwanza, Arusha, Moshi, Dar es Salaam and Dodoma attended the camp which conducted from June 7 to 21.

Dr Chandika explained that the Hospital performs bariatric surgery on people with excessive fat accumulation that may impair health and that the people who have failed to control obesity in normal ways including physical activity.

“Bariatric surgery therefore helps people with obesity to lose weight and lowers risk of medical problems associated with obesity,” he observed.

Long-term studies show the procedures cause significant long-term loss of weight, recovery from diabetes, improvement in cardiovascular risk factors, and a mortality reduction from 40 per cent to 23 per cent.

Dr Chandika informed that bariatric surgery is used to physically limit the amount of food the stomach can hold, which limits the number of calories one can eat and shorten or bypass part of the small intestine, which reduces the amount of calories and nutrients the body absorbs.

Obesity is most commonly caused by a combination of excessive food intake, lack of physical activity and genetic susceptibility. A few cases are caused primarily by genes, endocrine disorders, medications or mental disorder.

Ends…

Hospitali Mkapa yaanza upasuaji unene wa tumbo

WATU wenye unene uliozidi nchini sasa wana fursa ya kuwa na furaha baada ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kuanza kufanya upasuaji wa kupunguza unene. Upasuaji wa aina hii ni wa kupunguza unene wa tumbo au kwa kuondoa sehemu ya tumbo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk Alphonse Chandika, alibainisha hayo jana hapa kuwa hospitali hiyo ya umma kuwa tayari imeshafanya kwa mafanikio ya upasuaji huo kwa mtu mmoja aliyekuwa na unene uliozidi kiasi.

“Tumefanikiwa kufanya upasuaji wa kupunguza unene kwa kijana mmoja aliyekuwa na unene uliopitiliza na upasuaji huu tumeufanya jana kwa mafanikio makubwa,” alisema Dk Chandika wakati wa kuelezea kambi ya upasuaji wa matundu madogo.

Hospitali ya Benjamin Mkapa yenye vitanda takribani 400, iliendesha kambi ya upasuaji wa matundu madogo kwa watu wenye matatizo ya uzazi inayoisha leo. Katika kambi hiyo, takribani watu 500 kutoka Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Dodoma wamehudumiwa katika kambi hiyo ambayo ilianza Juni 7, mwaka huu.

Akifafanua zaidi, Dk Chandika alisema kuwa hospitali yake inaendesha upasuaji wa kupunguza unene kwa watu ambao wana mrudikano mkubwa wa mafuta mwilini ambayo yanatishia afya yao na ambao wameshindwa kudhibiti kwa njia za kawadia ya kupunguza unene na uzito uliozidi.

“Kwa hiyo upasuaji wa Bariatric huwasaidia watu wenye unene kupunguza uzito, mafuta yaliyozidi mwilini hivyo kuwanusuru na hatari za kiafya zinazotokana na mtu kuwa na unene uliozidi.” Tafiti za kitiba za muda mrefu zinaonesha kuwa upasuaji wa aina hiyo unasaidia mwenye matatizo hayo kupunguza unene hivyo kumuepusha na magonjwa yatokanayo kama vile kisukari, hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kupunguza vifo vya ghafla kwa asilimia 40 hadi asilimia 23.

Dk Chandika alisema upasuaji wa bariatric unatumika katika kupunguza kiasi cha chakula mwilini ambacho tumbo kinaweza kuhifadhi, na kupunguza idadi ya kalori ambayo mtu anaweza kula na kupungua sehemu ya utumbo mdogo, ambao hupunguza kiasi cha kalori na virutubisho vinavyofonzwa mwilini. Uzito na unene uliopitiliza umekuwa ukichangiwa na ulaji wa chakula kupita kiasi na kutofanya mazoezi ya mwili.

Copyright © 2020 - Benjamin Mkapa Hospital All rights reserved

Privacy Policy    |   Disclaimer   |    Sitemap   

English English Swahili Swahili