Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile
akiwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.
Charles Shija

HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

 

WAGONJWA SABA WAPANDIKIZWA FIGO BENJAMIN MKAPA

Hospitali ya Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza Figo jumla ya Wagonjwa saba tangu
ilipoanza kufanya huduma hiyo kwa kushirikiana na Madaktari kutoka shirika la afya la
Tokushukai lilopo nchi ya Japan.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kibingwa za magonjwa ya Figo
katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Idadi ya wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni
43, ambapo 38 wamepatiwa huduma hiyo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili na wagonjwa
watano(5) hospitali ya Benjamin Mkapa
“Hivi navyoongea tayari mgonjwa mmoja amekwishapandikizwa figo na ameshatoka salama,
yupo anaendelea kuangaliwa, lakini wana mpango wa kuwafanyia wengine wawili tutapokuwa
tumekamilisha hili tutakuwa na wagonjwa saba ambao wamefanyiwa hospitali hii” alisema Dkt.
Ndugulile.
Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa, Serikali imelenga kuhakikisha kwamba inawajengea
uwezo Wataalamu wa ndani kufanya upasuaji wa kibingwa ili waweze kuwahudumia
Watanzania bila msaada kutoka Wataalamu wa nje.
“lengo na kusudio ni kuhakikisha kwamba tunajenga uwezo wa ndani wa kuweza kufanya
upasuaji huu” Alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho
kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi
kwa ajili ya matibabu.
“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka wagonjwa nje
ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa. 80 mpaka
100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.”
alisema Dkt. Ndugulile
Aidha, Dkt. Ndugulile amewashukuru Wataalamu kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya
Japan kwa kujitoa na kuja kuwajengea uwezo Wataalamu wa ndani hali iliyosaidia kupunguza
kiasi kikubwa cha fedha ambacho hutumika kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wanaoenda
kutibiwa nje.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nimepita kuwashukuru na kuwapongeza, kwa sababu badala
ya kutusaidia sisi samaki, wenzetu wa Japan wameamua kutupatia sisi mishipi na kutufundisha
jinsi ya kujua naamini ujuzi huu utatusaidia sana ” alisema Dkt. Ndugulile.
Mwisho.

Copyright © 2020 - Benjamin Mkapa Hospital All rights reserved

Privacy Policy    |   Disclaimer   |    Sitemap   

English English Swahili Swahili