Kumbukumbu za Kitabibu Na Taarifa zA Afya.
Idara ya kumbukumbu za kitabibu na taarifa za Afya inatoa huduma ya kuandikisha wagonjwa, kuandaa taarifa za wagonjwa wa nje na waliolazwa, kulaza wagonjwa, kuomba vibali ya vipimo maalum pamoja na huduma maalum, kukagua kadi za bima na kujaza fomu za bima na pia kuonganisha wagonjwa na kliniki mbalimbali.
Awali Idara hii ilikua ikitumia mfumo wa kufungulia mafaili wagonjwa ili waweze kupata matibabu lakini kutokana na kasi ya teknolojia idara inaandikisha wagonjwa na kutunza taarifa zao online.
Idara ya kumbukumbu za kitabibu na taarifa za afya inahudumu sehemu tatu ambazo ni executive clinic, emergency medicine na phase one na kwa sasa idara inatarajia kutoa huduma phase two.