Idara ya Macho
Published on June 26, 2025

Ilianzishwa mwaka 2015, Idara ya Macho katika Hospitali ya Benjamin Mkapa imejikita katika kutoa huduma kamilifu za afya ya macho kwa watu wenye matatizo mbalimbali ya macho. Kutoka mwanzo wa idara hii yenye daktari mmoja wa macho, sasa imekua na kuwa kitengo kamili chenye uwezo wa kutoa huduma za kisasa za uchunguzi, tiba na upasuaji wa macho, pamoja na programu madhubuti za utoaji wa elimu na huduma kwa jamii.
Mpango wa ujenzi wa kituo maalum cha huduma za macho (stand-alone Eye Center) upo mbioni, ambao utaongeza uwezo wa idara kutoa huduma za kitaalamu zaidi pamoja na mafunzo ya wataalamu wa macho.
Huduma Kuu Zinazotolewa
1. Uchunguzi wa Macho (Consultations)
Tunafanya tathmini za kina kwa ajili ya kutambua na kutibu magonjwa mbalimbali ya macho kama vile:
- Mtoto wa jicho
- Glaucoma
- Uharibifu wa macho unaotokana na kisukari (diabetic retinopathy)
- Makosa ya kuona (refractive errors)
2. Upasuaji wa Macho
Tunatoa huduma za upasuaji ikiwemo:
- Uondoaji wa mtoto wa jicho kwa njia ya kisasa (kwa tundu dogo)
- Upasuaji wa macho kwa watoto
- Upasuaji wa Glaucoma
- Matibabu ya retina kwa kutumia mionzi (laser)
- Upasuaji wa kurekebisha matatizo maalum ya macho
3. Huduma za Macho kwa Watoto
Tunatibu matatizo ya macho kwa watoto ikiwemo:
- Mtoto wa jicho wa kuzaliwa nao
- Matatizo ya jicho kutotazama sawasawa (strabismus)
- Magonjwa mengine ya macho ya utotoni
4. Tiba za Macho za Kawaida
Huduma zetu za matibabu ya macho zinajumuisha:
- Matibabu ya maambukizi ya macho
- Matibabu ya macho makavu (dry eye syndrome)
- Tiba ya magonjwa ya kuzorota kwa retina (macular degeneration)
Huduma za Uchunguzi wa Kisasa
- Optical Coherence Tomography (OCT): Uchunguzi wa retina kwa picha zenye ubora wa hali ya juu
- Upimaji wa Miwani (Refraction Testing): Kutathmini hitaji la miwani
- Visual Field Test: Kuchunguza uwezo wa kuona pembeni (hasa kwa wagonjwa wa glaucoma)
- A/B Scan: Kupima kwa kutumia mawimbi ya sauti sehemu za ndani ya jicho
- Tonometry: Kupima presha ya ndani ya jicho
- Visual Function Analysis: Kuchambua uwezo wa kuona kwa ujumla
- Lane Park Unit with Phoropter: Kitengo maalum kwa ajili ya kupima na kurekebisha matatizo ya kuona kwa usahihi
Huduma za Kinga na Ushirikiano na Jamii
- Upimaji wa Macho Jamii: Tunafanya uchunguzi wa macho vijijini na maeneo ya mijini ili kugundua matatizo ya macho mapema
- Elimu kwa Umma: Kupitia semina, warsha na kampeni, tunatoa elimu ya afya ya macho na umuhimu wa uchunguzi wa mara kwa mara
- Uhamasishaji: Tunashirikiana na shule, sehemu za kazi na jamii kwa ujumla ili kukuza uelewa wa afya ya macho
Wataalamu na Utaalamu
- Madaktari Bingwa wa Macho (3): Hutoa huduma za kitaalamu za uchunguzi na upasuaji
- Madaktari wa Kawaida: Hushughulikia matatizo ya kawaida ya macho
- Wataalamu wa Miwani na Vifaa vya Macho: Hutoa huduma za upimaji wa macho na utoaji wa miwani
- Wauguzi wa Macho: Hushirikiana katika tiba, upasuaji na elimu kwa wagonjwa
- Timu ya Wataalamu Mbalimbali: Ushirikiano na wataalamu wa lishe, huduma za kijamii, na wahudumu wa afya kwa huduma jumuishi kwa mgonjwa
Miundombinu na Teknolojia
Idara inatumia vifaa vya kisasa kama vile:
- Mashine za OCT
- A/B Scans
- Visual Field Analyzers
- Phoropter (kwa upimaji wa kuona)
- Vifaa vya kupima presha ya jicho na kupima miwani
Maendeleo Yanayotarajiwa:
Ujenzi wa jengo maalum la huduma za macho utakuwa hatua muhimu katika kuwa kitovu cha huduma bora za macho kikanda.
Mafanikio Makubwa
- Idadi ya Wagonjwa: Tunahudumia maelfu ya wagonjwa kila mwaka, ikionesha mchango mkubwa wa idara katika jamii
- Upanuzi wa Huduma: Tumepanua huduma zetu kujumuisha elimu, uchunguzi wa mapema na tiba za kisasa
- Uboreshaji wa Miundombinu: Ukarabati wa vyumba vya upasuaji na ununuzi wa vifaa vya kisasa
- Karakana ya Miwani: Tuna karakana ya kisasa ya kutengeneza na kurekebisha miwani ndani ya Hospitali
Mipango ya Baadaye
- Kituo cha Umahiri cha Tiba za Macho: Kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Chuo Kikuu cha Dodoma, lengo ni kuanzisha kituo kikuu cha rufaa, utafiti na mafunzo ya macho
- Upanuzi wa Huduma za Kisasa: Kuboresha huduma za laser na kuongeza huduma za kibingwa
- Uboreshaji wa Outreach: Kupanua huduma vijijini na katika maeneo yasiyofikiwa kwa urahisi
- Maendeleo ya Rasilimali Watu: Mafunzo endelevu kwa wataalamu ili kuendelea kufikia viwango vya kimataifa
Established in 2015, the Eye Department at Benjamin Mkapa Hospital is dedicated to delivering comprehensive eye care services to individuals with diverse ocular conditions. From modest beginnings with a single ophthalmologist, the department has evolved into a fully-fledged unit offering advanced diagnostic, medical, and surgical eye care, along with impactful community outreach programs.
A stand-alone Eye Center is currently being planned to expand the department’s capacity for specialized care and training.
Core Services
1. Consultations
We provide in-depth evaluations for various eye conditions, including cataracts, glaucoma, diabetic retinopathy, and refractive errors.
2. Eye Surgery
We offer a range of surgical procedures such as:
- Cataract removal using small incision techniques
- Paediatric eye surgeries
- Glaucoma management surgeries
- Laser treatment for retinal diseases
- Corrective surgeries for specific vision impairments
3. Paediatric Eye Care
We manage and treat congenital and developmental eye conditions including congenital cataracts and strabismus.
4. Medical Eye Treatment
We offer tailored treatment for:
- Eye infections
- Dry eye syndrome
- Macular degeneration and other degenerative conditions
Advanced Diagnostic Services
- Optical Coherence Tomography (OCT): For high-resolution retinal imaging
- Refraction Testing: To determine corrective lens prescriptions
- Visual Field Assessment: For peripheral vision testing (e.g., glaucoma detection)
- A/B Scans: Ultrasonography of internal eye structures
- Tonometry: For intraocular pressure measurement
- Visual Function Analysis
- Lane Park Refraction Unit with Phoropter: For accurate vision assessment and correction
Preventive Services and Community Engagement
- Eye Screening Programs: Conducted in communities to detect cataracts, refractive errors, and other vision issues early
- Health Education Campaigns: Including seminars, school visits, and public workshops on eye health and hygiene
- Awareness Outreach: Engaging communities, schools, and workplaces in promoting routine eye exams and early intervention
Staff and Expertise
- Senior Ophthalmologists (3): Providing expert diagnosis and surgery
- Medical Officers: Handling general eye cases and follow-ups
- Optometrists & Technicians: Delivering vision assessments and eyewear support
- Ophthalmic Nurses: Supporting treatment, surgery, and patient education
- Multidisciplinary Team: Collaboration with social workers, nutritionists, and other specialists for holistic patient care
Facilities and Technology
The department is equipped with:
- OCT machines
- A/B Scans
- Visual field analyzers
- Phoropter-equipped Lane Park units
- Tonometry and refraction devices
Planned Development: A dedicated Eye Care Building is set for construction to serve as a regional hub for advanced ophthalmic services.
Achievements and Milestones
- Patient Volume: Serving thousands annually with growing demand
- Service Growth: Expanded focus to include community education, early detection, and high-level diagnostics
- Infrastructure Improvements: Renovation of operating theatres, procurement of state-of-the-art equipment
- Eyeglass Workshop: Operational on-site facility for frame fitting and lens fabrication
Future Plans
- Center of Excellence for Vision Care: In collaboration with the Ministry of Health and UDOM, aiming to position BMH as a regional referral center
- Expansion of Advanced Treatment: Including more laser interventions and sub-specialist services
- Enhanced Outreach Programs: Targeting rural and underserved communities
- Capacity Building: Continuous professional development for staff to ensure adherence to international standards
Â