Mwanzo / Kurasa / Utafiti na Ubunifu

Utafiti na Ubunifu

Published on June 27, 2025

Article cover image

Kitengo cha Utafiti  na Ubunifu ni nguzo muhimu katika kukuza maarifa ya kisayansi, kuimarisha mifumo ya afya, na kuboresha huduma za wagonjwa kupitia tafiti za kisasa. Kitengo hiki kinasimamia, kuratibu na kuwezesha shughuli zote za utafiti ndani ya hospitali au kwa ushirikiano na wadau wa nje.

Malengo ya kitengo ni kuhakikisha maadili ya tafiti, ubunifu na uadilifu wa kisayansi vinazingatiwa, sambamba na kuhimiza maboresho ya huduma za afya kwa kutumia ushahidi wa kisayansi. Kinaboresha mara kwa mara sera za utafiti za hospitali ili ziendane na viwango vya kitaifa na kimataifa, pamoja na kusimamia mchakato wa mapitio ya maadili ya tafiti kupitia Bodi ya Taasisi   ya Maadili ya Utafiti  (IRB).

Dira

Kuwa hospitali ya kisasa inayotumia sayansi mpya kwa ajili ya jamii yenye afya na maendeleo endelevu kupitia tafiti bunifu.

Dhamira

Kuongoza, kuratibu na kusaidia tafiti za kliniki na ubunifu zenye matokeo chanya  kwa kuzingatia maadili, kukuza uwezo, kuhamasisha ushirikiano na  kutumia matokeo ya tafiti kuboresha afya ya jamii.

Majukumu Muhimu

  • Kuratibu tafiti za ndani na nje zinazofanyika BMH
  • Kusaidia na kusimamia watumishi wa hospitali katika utekelezaji wa tafiti, mafunzo ya tafiti, uwasilishaji wa tafiti kwenye mikutano ya kisayansi, uchapishaji na matumizi ya matokeo
  • Kuratibu utoaji wa vibali vya utafiti kwa tafiti za nje zinazofanyika BMH
  • Kuandaa na kuboresha  SOPs, sera, mikakati na miongozo ya utafiti ya BMH
  • Kusimamia maadili ya utafiti na mwenendo wa tafiti
  • Kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya utafiti
  • Kusimamia utekelezaji wa miradi ya utafiti
  • Kuanzisha na kuendeleza miundombinu ya utafiti, ikiwa ni pamoja na IRB na “registry” ya utafiti
  • Kuanzisha na kuimarisha mitandao ya ushirikiano wa utafiti
  • Kuandaa mwongozo wa ushauri elekezi (consultancy guideline)

Mafanikio na Hatua Muhimu

  • Kuandaa Sera ya Utafiti,”format” ya utafiti, na SOPs kwa ajili ya BMH na washirika wake
  • Kuanzisha mfumo wa kutangaza wito wa tafiti kwa watumishi wa BMH kwa kutumia fedha za mfuko wa ndani zilizotengwa kwa tafiti
  • Kuanzisha mfumo wa uwasilishaji na uchambuzi wa machapisho ya tafiti katika ngazi ya idara
  • Kusambaza matokeo ya tafiti kupitia maonyesho ya mabango, mawasilisho na matumizi ya matokeo ili kuboresha huduma
  • Kufanya na kuchapisha tafiti ambazo zinapatikana katika tovuti rasmi ya hospitali ambayo ni https://www.bmh.or.tz/publications/research
  • Kuanzisha vipindi vya mafunzo ya Utafiti kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa BMH kwa njia ya kuhudhuria ana kwa ana,pamoja na njia ya mtandao,vipindi hivi vinapatikana kupitia https://youtube.com/@bmhzoomsessions
  • Kuandaa warsha kadhaa za uandishi wa miradi na maombi ya ufadhili kwa kushirikiana na NHIR, Conservation, Food and Health Foundation, UNFPA, WHO, na NIC
  • Kupata ufadhili mdogo kutoka WHO na NIC kwa ajili ya kuanzisha huduma za Ukatili wa Kijinsia (GBV) na Ukatili dhidi ya Watoto (VAC), ikiwa ni pamoja na mafunzo, utayarishaji wa miongozo, huduma mkoba , na matangazo ya huduma husika yanayoruka katika Televisheni za Hospital, pamoja na mabango yaliyopo katika sehemu mbalimbali za Hospitali.
  • Kushiriki na kuwasilisha tafiti katika mikutano ya kisayansi, mfano mikutano ya kisayansi ya  MUHAS, UDOM, TANNA, NIMR, RMNCAH, Tanzania Health Summit na Mkutano wa Sayansi wa Huduma za Afya ya Msingi
  • Kuanzisha kundi la hiari la WhatsApp kwa watumishi wa BMH wanaopenda tafiti na miradi kwa ajili ya kubadilishana taarifa.

Watumishi na Utaalamu

  • Mtaalamu wa Afya ya Jamii
  • Mtaalamu wa Takwimu za Afya na Mtaalamu wa Magonjwa ya Mlipuko (Biostatistician & Epidemiologist)

Mipango inaendelea ili kupanua timu hii kwa kuajili  wataalamu watafiti katika “clinical trial”  , maafisa wa miradi, wataalamu wa ufuatiliaji na tathmini, na wataalamu wa data.

Mipango ya Baadaye

Sehemu inalenga kujenga mazingira jumuishi, bunifu, na yenye tija ya utafiti ndani ya BMH. Vipaumbele vya kimkakati vya baadaye ni pamoja na:

  • Kukamilisha na kuanza kutumia Daftari la Tafiti (Research Registry) la BMH
  • Kuimarisha na kupanua Bodi ya Maadili ya Utafiti (IRB)-BMH kwa kushirikiana na Bodi ya Maadili ya Utafiti (IRB) ya UDOM
  • Kuimarisha ushirikiano wa ndani ya nchi na kimataifa katika masuala ya utafiti na miradi
  • Kuendeleza mafunzo ya kujenga uwezo na programu za ushauri elekezi katika utafiti
  • Kujumuisha suluhisho za kisasa za AI katika tafiti na uchambuzi wa data
  • Kutumia njia za kidigitali katika mchakato wa utafiti (Digitization of research processes)
  • Kuanza majaribio ya kliniki (Clinical Trials) na kupanua tafiti shirikishi
  • Kuimarisha utekelezaji na uwakilishi wa utafiti katika kila idara za Hospitali
  • Kuajiri wataalamu wa utafiti kutoka fani mbalimbali
  • Kupanua utekelezaji wa utafutaji na usimamizi wa miradi ya utafiti

Jiunge Nasi

Tunakaribisha ushirikiano na taasisi, watafiti, wafadhili, na wadau watakaopenda kushirikiana nasi kwenye utafiti, ubunifu na miradi. Kwa pamoja, tunaweza kujenga mustakabali bora wa afya kupitia tafiti zenye ushirikiano, ubunifu na zenye matokeo chanya kwa jamii. Tufikie kupitia barua pepe; research@bmh.or.tz

Unaweza pia kutuandikia wazo la utafiti unaopendekeza ufanyike BMH, kupitia barua pepe; research@bmh.or.tz