Sehemu ya Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu
Published on August 13, 2022

Idara ya Magonjwa ya Moyo na Upasuaji wa Moyo na Kifua katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imeendelea kukua kwa hatua tangu kuanzishwa kwa hospitali mwaka 2015. Hapo awali, huduma zilikuwa zikitolewa na daktari bingwa mmoja wa magonjwa ya moyo kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma. Katika kipindi hicho, idara ilijikita zaidi kwenye uchunguzi usiohusisha upasuaji (non-invasive diagnostics), ikiweka msingi wa maboresho ya baadaye.
Mwaka 2019, idara ilifikia hatua muhimu kwa kuanza upasuaji wa moyo wazi kwa watoto pamoja na uzinduzi wa maabara ya kateteri (catheterization laboratory). Mafanikio haya yalitokana na juhudi za daktari bingwa wa moyo na daktari bingwa wa upasuaji wa kifua waliopo hospitalini, kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na wataalamu wa kimataifa waliokuwa sehemu ya ushirikiano wa hospitali shirika.
Kwa msingi huo, BMH iliongeza uwezo wake zaidi mwaka 2022 kwa kuanzisha upasuaji wa moyo wazi kwa watu wazima. Hivi sasa, idara hii ina vifaa vya kisasa na timu ya wataalamu wa fani mbalimbali waliobobea, inayotoa huduma za kina za magonjwa ya moyo. Maendeleo haya yanadhihirisha dhamira ya BMH ya kuwa kituo kinachoongoza katika huduma za moyo na upasuaji wa kifua nchini Tanzania.
Huduma Zitolewazo
Kliniki za wagonjwa wa nje:
- Kliniki ya jumla ya magonjwa ya moyo inayoendeshwa siku 6 kwa wiki na kuhudumia takribani wagonjwa 25,000 kwa mwaka
- Kliniki ya upasuaji wa moyo, kifua na mishipa ya damu inahudumia takribani wagonjwa 500 kwa mwaka
Huduma kwa wagonjwa wa ndani:
- Huduma kwa wagonjwa waliolazwa kwa matatizo mbalimbali ya moyo kama vile:
ü Kushindwa kwa moyo (heart failure)
ü Mshtuko wa moyo wa ghafla (acute myocardial infarction)
ü Ugonjwa wa mapafu wa ghafla (acute pulmonary embolism)
ü Shinikizo la damu kali (malignant hypertension)
ü Huduma baada ya matibabu ya moyo
ü Idara huhudumia takribani wagonjwa 600 kwa mwaka
Vipimo vya Uchunguzi
Vipimo visivyoingilia (Non-invasive):
- “ECG” ya msitari 12
- “Holter monitoring” ya saa 24/48
- “Ambulatory Blood Pressure (ABP) monitoring” ya saa 24/48
- Stress ECG (treadmill test)
- “Echocardiogram” ya kawaida na ya juu kama vile “dobutamine stress ECHO” na “transesophageal ECHO”
- Kwa mwaka 2023, vipimo visivyoingilia takribani 3,000 vilifanyika
Taratibu za uchunguzi zinazoingilia (Invasive procedures):
- Kateteri ya moyo kulia na kushoto kwa uchunguzi (diagnostic right and left catheterization)
- Upanuzi wa mishipa ya moyo (Percutaneous Coronary Angioplasty)
- Kufunga vifaa kwa magonjwa ya kimuundo ya moyo (ASD, PDA, VSD)
Taratibu za Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu
- Kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (Coronary Artery Bypass Grafts)
- Kuunda fistula ya arteriovenous kwa ajili ya hemodialysis
- Kuweka katheta ya kudumu kwa ajili ya hemodialysis
- Kufunga na kuondoa mishipa ya “varicose”
- Sclerotherapy kwa mishipa ya varicose, pamoja na kuondoa aneurysm
- Thrombo-embolectomy (kuondoa damu iliyoganda)
- Upasuaji wa bypass ya “femoral-popliteal”
- Kubadilisha na kutengeneza valvu za moyo
- Upasuaji wa mapafu (lung resection)
- Kuondoa uvimbe wa kifua na mediastinali
- Upasuaji wa mishipa ya shingo (Carotid Endarterectomy)
Vifaa Vilivyopo
- Mashine tatu za “ECG” zenye msitari 12
- Mashine 3 za “echo”
- Vifaa vya “Holter” na “ABP”
- Mashine 1 ya “stress ECG” (treadmill)
- Maabara 1 ya “Cathlab” ya moyo
Miundombinu Iliyopo
- Maabara ya “Echo”
- Chumba cha vifaa vya moyo
- Kitengo cha uangalizi maalum wa moyo (Coronary Care Unit) chenye vitanda 9
- Vyumba 7 vya kliniki kwa ajili ya mashauriano
- Wodi maalum kwa ajili ya wagonjwa wa moyoRaslimali Watu