Idara ya Ustawi wa Jamii

Utangulizi:
Idara ya Ustawi wa Jamii ni kati ya idara ndani ya Hospitali ya Benjamin Mkapa. Idara inatoa huduma za Amara Jamii (Social Work) ambazo ndio msingi mkuu wa huduma za Ustawi wa Jamii katika mahitaji mbali mbali na maeneo ya huduma za matibabu tofauti. Kazi kuu ya wataalamu wa Amara Jamii (Social workers) ni kusaidia Wagonjwa na familia zao au wateja kuweza kumudu athari zitokanazo na ugonjwa /magonjwa wakati wa matibabu na jinsi ya kuishi baada ya mabadiliko ya kiafya. Miongoni mwa huduma kuu zaidi katika idara ni pamoja na;
• Tathmini ya hali ya Kisaikolojia kwa wagonjwa na familia zao
• Unasihi na Tiba saikologia (Counseling & Psychotherapy):
• Elimu kwa Wagonjwa na Familia:
• Ushauri wa rasilimali na mpango wa kurudisha wagonjwa nyumbani baada ya matibabu (Resource Counseling and Discharge Planning):
• Msaada kwa wagonjwa wa nje (Supportive Care to Outpatients):
• Huduma za malalamiko (Complaints Services)
Huduma za Ustawi wa Jamii zilizofikiwa na Mafanikio yake:
MWAKA |
Kusikiliza na kutambua mahitaji ya wagonjwa/wateja |
Hafua za msaada na tiba saikolojia kwa wagonjwa/ wateja na familia zao |
Malalamiko yaliyopokelewa na kutatuliwa |
Wagonjwa waliopatiwa msaada wa matibabu |
2021/2022 |
12,000 |
754 |
35 |
2,181 |
2022/2023 |
11,622 |
665 |
38 |
2,652 |
2023/2024 |
12,877 |
908 |
44 |
2,234 |
2024/2025 Machi |
9,412 |
868 |
39 |
1,811 |
Jumla kuu |
45,911 |
3,195 |
156 |
8,878 |