Idara ya Lishe na Chakula

Published: Sep 10, 2025
Idara ya Lishe na Chakula cover image

Utangulizi:

Idara ya Tiba Lishe ni kati ya idara zilizopo katika kurugenzi ya Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa. Idara inatoa huduma mbalimbali za matibabu lishe kwa wateja kulingana na mahitaji yao baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari na wataalamu wa Lishe.

 Huduma zinazotolewa na idara ya Tiba Lishe ni pamoja na;

1. Kufanya tahimini ya hali ya lishe kwa wateja wetu

2. Kutoa matibabu ya lishe kutokana na tatizo la mgonjwa

3. Kuandaa mpangilio wa chakula kutokana na hitaji la mteja

4. Kufuatilia wateja wetu kutokana na ushauri waliopewa

5. Kutoa ushauri wa lishe kwa wateja wetu

6. Kutoa elimu ya lishe bora kwa wateja wetu

7. Kutoa huduma za lishe kwa makundi maalumu

8. Kufanya tafiti ya masuala ya lishe

 

Mafanikio ya Idara ya Tiba Lishe

1. Kuanzishwa kwa idara ya Tiba Lishe katika hospitali ya Benjamin

2. Kupata watumishi wa ajira ya kudumu wanne (4)

3. Kupata ofisi na samani za ofisi

4. Kuongezeka kwa idadi wa wateja kutoka 537 mwaka 2021/2022 mpaka 3,900 mwaka 2024/.

Kwa maelezo zaidi piga; +255784391070