Sehemu ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake
Published on June 30, 2025
Idara inatoa huduma mbalimbali katika fani ya uzazi na magonjwa ya wanawake, zikiwemo:
- Huduma za Ushauri na Uchunguzi: Kuchunguza na kutibu matatizo kama vile
- Mabadiliko yasiyo ya kawaida ya hedhi
- Endometriosis
- Ugumba
- PID (Pelvic Inflammatory Disease)
- Polycystic Ovarian Syndrome
- Antiphospholipid Syndrome
- Huduma za Upasuaji: Kufanya upasuaji mbalimbali kama vile:
- Kuondoa uvimbe wa mji wa mimba (Myomectomy)
- Upasuaji wa kumtoa mtoto kwa njia ya upasuaji (Caesarean Section)
- Kufungua mirija ya uzazi (Tubal Plasty)
- Kuondoa mji wa mimba kwa njia ya tumbo (Total Abdominal Hysterectomy)
- Upasuaji wa matundu madogo (Laparoscopic Surgeries)
- Huduma za Uchunguzi: Kutumia teknolojia ya kisasa katika uchunguzi wa matatizo, ikiwa ni pamoja na:
- Uchunguzi wa kwa kutumia laparoscope
- Uchunguzi wa kwa kutumia hysteroscope
- Picha za uchunguzi kwa usahihi wa hali ya mgonjwa
- Huduma za Kinga na Uhamasishaji:
- Elimu ya afya kwa jamii kuhusu magonjwa ya wanawake
- Uhamasishaji juu ya afya ya uzazi na changamoto za ugumba
Watumishi wa Idara:
Idara ina timu yenye weledi na dhamira ya kutoa huduma bora, inayojumuisha:
- Madaktari Bingwa: Wapo madaktari bingwa 8 wa uzazi na magonjwa ya wanawake pamoja na madaktari 2 wa kawaida
- Watoa Huduma Wasaidizi: Wauguzi na wataalamu wengine wanaoshirikiana kwa karibu kuhakikisha mgonjwa anapata huduma kamili
Mipango ya Baadaye:
Idara imejipanga kupanua huduma na miundombinu yake, ikiwa ni pamoja na:
- Ujenzi wa Jengo Maalum: Mpango wa kujenga jengo la kujitegemea kwa ajili ya huduma maalum za uzazi na wanawake, kulingana na mpango mkuu wa taasisi
- Huduma za Kibingwa Zaidi: Baadhi ya huduma za kibingwa tayari zimeanza, huku huduma nyingine zikisubiri wataalamu walioko masomoni kurejea
- Upanuzi wa Elimu kwa Jamii: Kupanua huduma za uchunguzi na elimu ya afya hadi katika maeneo yenye uhitaji mkubwa
- Mafunzo Endelevu kwa Wafanyakazi: Kuwezesha timu ya idara kuendelea kujifunza na kufahamu maendeleo ya hivi karibuni katika fani ya uzazi, magonjwa ya wanawake, na tiba ya ugumba
Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Benjamin Mkapa inabaki kuwa nguzo muhimu katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wanawake nchini, na inaendelea kupanua wigo wa huduma kwa lengo la kuongeza ufanisi, upatikanaji, na ustawi wa jamii.