Kuhusu Huduma za Tiba
Published on July 04, 2025
Karibu Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Mimi ni Dkt. Kessy Charles Shija, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, niliye bobea katika huduma za Upandikizaji wa Figo.
Kurugenzi ya Huduma za Tiba katika Hospitali ya Benjamin Mkapa inatoa huduma za matibabu ya msingi na za kibingwa kupitia idara zifuatazo:
-
Idara ya Watoto na Afya ya Mtoto
-
Idara ya Tiba ya Ndani na Magonjwa ya Mfumo wa Chakula
-
Huduma za Figo (Urologia na Nefrologia)
-
Idara ya Moyo na Upasuaji wa Moyo na Kifua
-
Idara ya Magonjwa ya Damu, Saratani na Tiba ya Nyuklia
-
Tiba Rehabilitishi na Afya ya Akili
Tangu ilipozinduliwa mwaka 2015, hospitali hii imepiga hatua kubwa kupitia uwekezaji wa kimkakati katika teknolojia za kisasa za kitabibu. Baadhi ya mafanikio makubwa yaliyochagizwa na Kurugenzi ya Huduma za Tiba ni pamoja na:
-
Kuanzishwa kwa huduma za Haemodialysis na Upandikizaji wa Figo (2018)
-
Huduma za Cardiac Catheterization (2019)
-
External Shock Wave Lithotripsy (2019)
-
Huduma za Gastroenterolojia ya Uchunguzi na Uingiliaji (2019)
-
Laser Lithotripsy (2020)
-
Upasuaji wa Moyo wa Watoto (2021)
-
Huduma za Neonatolojia (2022)
-
Upasuaji wa Moyo kwa Watu Wazima (2023)
-
Upandikizaji wa Uboho (Bone Marrow Transplantation) (2023)
Mafanikio haya yamewezeshwa kupitia juhudi za ndani na ushirikiano wa kimkakati na taasisi za kitaifa na kimataifa. Baadhi ya ushirikiano huo ni:
-
Upandikizaji wa Figo: Kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma na Tokushukai Medical Group
-
Huduma za Moyo (Catheterization na Upasuaji wa Moyo): Kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma, Jakaya Kikwete Cardiac Institute, ZGT Overzee (Uholanzi), Heart and Soul (Marekani), na Save a Child’s Heart (Kuwait)
-
Upandikizaji wa Uboho: Kwa kushirikiana na taasisi ya HELLP3 kutoka Italia
Asante kwa kuendelea kuiamini Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Katika Kurugenzi ya Huduma za Tiba, tumejizatiti kuendelea kutoa huduma bora, za kitaalamu na zenye kumlenga mgonjwa.