Ushirikiano wa Ndani
Published on June 27, 2025
Hospitali ya Benjamin Mkapa ina ushirikiano na wadau mbalimbali wa ndani na wa kimataifa. Washirika wa ndani wa hospitali ni pamoja na: Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya (MZRH), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (DRRH) na shirika la Light for the World.
Ushirikiano huu umechangia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza huduma za moyo na upasuaji wa moyo na kifua (Cardiology na Cardiothoracic surgery), huduma kwa wagonjwa mahututi (ICU), upasuaji, na huduma za macho (Ophthalmology) kupitia ujenzi wa uwezo kwa wataalamu wa kutoa huduma hizo.