Huduma za Uuguzi
Published on July 01, 2025

Kurugenzi ya Uuguzi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ilianzishwa mwaka 2015 mara tu hospitali ilipoanzishwa. Ilianza na wauguzi 17 ambao walihamishwa kutoka hospitali ya mkoa wa Dodoma na baadae waliongezeka kutoka mikoa mbalimbali pamoja na Wizara ya afya.
Kurugenzi ilianza na idara moja ambayo ilikuwa ni Housekeeping and Laundry ambayo iliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi. Kurugenzi iliendelea kukua hadi kufikia kuwa na idara 5 kwa sasa ambazo ni “Housekeeping and laundry”, “Theatre complex”, “Central sterilization”, “Social welfare” na “Food and nutrition”.
Jumla ya wagojwa 232,049 walitibiwa kwa kipindi cha mwaka 2024/2025 ikiwa ni ongezeko la wagonjwa 62,436 ikilinganishwa na wagonjwa 169,613 ambao walitibiwa katika kipindi cha mwaka 2020/2021.
Majukumu ya kila Idara.
Idara ya “Housekeeping and Laundry”:
Huduma za wagonjwa wa nje:
Tunazo Kliniki za magonjwa ya ndani na upasuaji, Kliniki ya uzazi na magonjwa ya kina mama, Kliniki ya watoto, Kliniki ya magonjwa ya dharura (EMD), kitengo cha mazoezi ya viungo (Physiotherapy) na huduma zote za ubingwa na ubingwa bobezi zinapatikana katika Kliniki zetu. Huduma zetu za Kliniki za kawaida zinatolewa kila siku za kazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:30 mchana. Jumamosi Klinikii zinaanza saa 2:00 hadi saa 7:00 Mchana. Jumapili idara ya magonjwa ya dharula inatoa huduma masaa 24 kwa siku 7 kwa ajili ya kuona wagonjwa wenye dharula mbalimbali. Huduma hizi hutolewa na wauguzi wenye ujuzi na weledi wa hali ya juu na kumfanya mgonjwa kuwa katika hali ya amani na utulivu.Pia tunatoa huduma za “Executive Clinic” kwa viongozi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni, Pia kuna Klinikii za “Fast track” na Master health checkup ambazo zinaanza saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku siku za kazi na siku za mwisho wa wiki ni kama ilivyo hapo juu.
Huduma za wagonjwa wa ndani(IPD)
Tuna wodi za kawaida nzuri na za kisasa ambazo zina vitanda 3 hadi 5, wauguzi wenye utaalamu wa kutosha unaomfanya mgonjwa kujisikia amani na utulivu, huduma za uuguzi hujumuisha aina mbalimbali za uangalizi wa wagonjwa, ikiwa ni pamoja na huduma za matibabu ya magonjwa ya ndani na upasuaji, huduma za elimu ya afya na ushauri nasaha, huduma bora kwa mteja inayohusisha lugha nzuri na huduma za staha na utu. Wauguzi pia wana jukumu la kupanga namna ya kumruhusu mgonjwa kwenda nyumbani baada ya kupona wakishirikiana na watumishi wengine wa kada mbalimbali ndani ya hospitali.
Huduma maalum za Uuguzi:
Tunatoa huduma za Uuguzi kwa wagonjwa wa kupandikiza uroto, uchujaji damu (dialysis), huduma za magonjwa ya moyo na mishipa, huduma za wagonjwa wa saratani, Huduma za magonjwa ya figo, Huduma za Uzazi na magonjwa ya kina mama, Huduma za watoto na watoto wachanga, Huduma za vipimo mbalimbali, matibabu ya masikio, pua na koo, matibabu ya macho na huduma zote za kiuguzi katika ubora wa hali ya juu.
WADI ZA VIP NA “PRIVATE”:
Tunatoa huduma za vyumba vya VIP na “Private” kwa wagonjwa wanaohitaji vyumba hivi. Kuna jumla ya vyumba 42 vya VIP na “Private”, Vyumba hivi vya VIP na “Private” ni vyumba binafsi vya kujitegemea vyenye ukubwa wa kutosha na samani za ndani.
Wagonjwa katika wodi za VIP na “Private” wanapatiwa huduma za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wanaohusika na ugonjwa husika, yaani magonjwa ya ndani na upasuaji. Matibabu katika wodi za VIP na “Private” yanafuata utaratibu wa “Fast track” yaani matibabu ya haraka kwa kila idara, vipimo vya maabara pamoja na “Emergence”. Kuna huduma zingine za kijamii ambazo zinatolewa katika wodi hizi, pamoja na huduma za “WiFi”.
Huduma za Uuguzi katika vyumba vya upasuaji:
Kuna vyumba 11 vya upasuaji, ambavyo vinafanya upasuaji wa magonjwa ya matumbo, mifupa, mishipa, upasuaji wa magonjwa ya moyo, uzazi na magonjwa ya wanawake, njia ya mkojo, masikio, pua na koo, macho,upandikizaji uroto na figo.Tunatoa tathmini kwa wagonjwa wetu, kuwaeleza taratibu za upasuaji, na kuwatayarisha kwa ajili ya upasuaji, kuhakikisha wanaelewa hatari na manufaa ya upasuaji unaoenda kufanyika.
Wauguzi huandaa wagonjwa kabla ya upasuaji, hutayarisha vifaa, na kufuatilia wagonjwa wakati wote wa mchakato wa anesthesia, husaidia daktari wakati wa upasuaji na kudhibiti vifaa vyote vinavyohitajika wakati wa upasuaji na hutoa huduma za usaidizi baada ya anesthesia na upasuaji, kufuatilia jinsi wanavyopona kutoka kwenye anesthesia na kuhakikisha kwamba wanaweza kuruhusiwa kurudi kwenye wadi.
Kitengo cha utakasaji:
Katika hospitali yetu, kuna idara ya utakasaji ambayo ina jukumu kubwa na muhimu katika kuhakikisha usalama wa mgonjwa kwa kutoa vifaa na vifaa tiba vinavyoweza kutumika kwa mara nyingine baada ya kutakaswa.Vifaa hivi hutakaswa kwa kutumia “autoclave” na gesi. Utaratibu huu husaidia kuzuia kuenea kwa maambukizi kwa kuteketeza wadudu wa aina mbalimbali na kuhakikisha kuwa vifaa vinakuwa salama kwa matumizi na kugawanywa ndani ya vyumba vya upasuaji.
Wauguzi maalum:
Kurugenzi ya Uuguzi ina wauguzi waliobobea katika kansa, figo, moyo na mishipa, Ukunga, magonjwa ya watoto na Afya ya jamii.
Kurugenzi ina wauguzi ambao wanasaidia katika uangalizi wa wagonjwa muda wote na ni wale ambao wana ujuzi maalum kwa uangalizi wa magonjwa yaliyoorodheshwa hapo juu.
Ushirikiano na kada zingine:
Kurugenzi ya Uuguzi inafanya kazi kwa kushirikiana na Kurugenzi ya Utawala na Rasilimali Watu, Mipango na Fedha,Upasuaji,magonjwa ya ndani, Huduma shirikishi,mafunzo na Utafiti, Kitengo cha Ununuzi, kitengo cha Habari na Tehama.Ushirikiano huu ni lengo moja tu, kukidhi mahitaji ya mgonjwa na kutoa huduma bora yenye kiwango cha juu.
Majengo na vifaa:
-
Tunatoa huduma za kulaza wagonjwa katika wodi za aina mbalimbali ambazo ni VIP, “Private””na semi “Private”. Lakini pia tuna wodi za kawaida ambazo ni nzuri sana.
-
Upanuzi wa vyumba vya VIP: Kutokana na uhitaji mkubwa wa vyumba vya VIP, ukarabati unaendelea ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa na wateja wetu.
Moja ya Vyumba vya "Private" BMH
Mafanikio:
-
Kwa sasa hospitali inapokea wagonjwa wa nje 1000 hadi 1200 kwa siku. Wagonjwa waliolazwa wodini ni 250 hadi 270 kwa siku, wagonjwa wanaolazwa kwa siku ni 50 hadi 70 kwa siku.
Mipango ya baadae:
-
Kuongeza vyumba vya VIP: Tunatarajia kuongeza vyumba vya VIP na “Private” hadi kufikia vyumba 70 au zaidi ili kuendana na mahitaji ya wagonjwa na wateja wetu ambao huwa wanahitaji vyumba hivyo.
-
Kuongeza Wauguzi bingwa. Tuna mpango wa kusomesha wauguzi katika fani za magonjwa ya “Critical Care”, “Endoscopic services”, “Cardiovascular”, “Nephrology”, “Neonatology”, “Midwifery”, “Pediatrics”, na nyinginezo.
-
Kuongeza maeneo ya matibabu: Tuna mpango wa kuanzisha huduma za home based care ili kusogeza huduma karibu na wateja walipo.
-
Huduma za uzazi: Tunatarajia kuanzisha huduma mpya za uzazi shirikishi kati ya mzazi na mwenza au ndugu mwingine. (labor and delivery services companionship).
Maendeleo ya Wauguzi:
kuendeleza wauguzi katika mafunzo ya muda mfupi, kielimu (CPD), “attachment” pamoja na “Observation learning” ili kuendana na maendeleo ya technolojia mpya na matumizi ya mashine na vifaa tiba vya kisasa ambavyo vinaendana na hospitali yetu.