Wodi
WODI YA UPASUAJI NA MFUMO WA MKOJO
Wodi hizi zinapatikana jengo la pili (phase 2) katika ghorofa namba moja (first floor), Ghorofa namba moja inahusika kulaza wagonjwa wenye shida ya upasuaji na mfumo wa mkojo.
WODI YA MAGONJWA YA NDANI (WANAWAKE NA WANAUME), MAGONJWA YA FIGO, WATOTO WADOGO, MIFUPA NA MISHIPA YA FAHAMU NA SARATANI.
Wodi hizi zote zinapatikana jengo la pili ghorofa namba mbili.
WODI YA WAKINA MAMA WAJAWAZITO
Wodi ya wakina mama wajawazito nayo inapatikana jengo la pili ghorofa namba tatu.
WODI YA VIONGOZI NA WATU BINAFSI
Wodi ya viongozi na watu binafsi inapatikana jengo la pili ghorofa namba nne.
WODI YA WAGONJWA MAHUTUTI
Wodi ya wagonjwa mahututi hii ni wodi ambayo inapatikana jengo la kwanza mkabala na kliniki ya saratani ghorofa ya kwanza
WODI YA WAGONJWA MAHUTUTI WA MOYO
Wodi ya wagonjwa mahututi wa moyo nayo inapatikana jengo la kwanza ghorofa namba moja, wodi hii iko karibu na kliniki ya magonjwa ya moyo.