Upandikizaji wa Figo
Hospitali ya Benjamin Mkapa imeanza kutoa huduma ya upandikizaji figo kwa wagonjwa wenye shida na matatizo ya figo. Uongozi wa Benjamin mkapa unapenda kuwataarifu wateja wake wote kuwa hospitali hiyo imeanza na mkakati wa kupandikiza figo kwa kutumia madaktari wazawa
Huduma hii itawasaidia wananchi kuepusha gharama za uasafiri kusafiri nje ya nji kwa ajili ya kutafuta huduma hii kama ilivyokuwa hapo mwanzo. Mkurugenzi mtendaji ameongea na vyombo vya habari na kutoa taarifa hiyo na kuwaomba watanzania wote wenye shida ya figo kuja kupata matibabu katika hospitali ya Benjamin Mkapa.