Mwanzo / Huduma Zetu / Hospitali ya Benjamin Mkapa yazindua Huduma za Wagonjwa wa Kimataifa na Tiba Utalii.

Hospitali ya Benjamin Mkapa yazindua Huduma za Wagonjwa wa Kimataifa na Tiba Utalii.

Published on July 11, 2025

Article cover image

Dodoma, 10 April 2025.

Waziri wa Afya, Mheshimiwa Jenista Mhagama , leo amezindua huduma za wagonjwa wa Kimataifa na tiba utalii katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) jijini Dodoma. Huduma hizo zitatolewa kwa wagonjwa wa kigeni wanaotoka nje na ndani ya nchi ;Niwapongeze sana Uongozi wa BMH kwa ubunifu huu na mnatekeleza maono ya Mheshimiwa Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan ya kuchochea tiba utalii nchini” amesema Mhe Mhagama. 

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa BMH alieleza kuwa kliniki ya huduma hizo itaweza kuhudumia wagonjwa 100 k kwa siku na ina ubora wa hali ya juu wa kimataifa na wenye faida za ziada kama mazingira mazuri, sehemu nzuri za kupumuzika , kupata vinywaji laini, mtandao na zenye kufanya mgonjwa atibiwe ndani ya muda mfupi.