BMH KUTAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA HUDUMA ZA MATIBABU YA KIBOBEZI

Published: Dec 10, 2025
BMH KUTAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA HUDUMA ZA MATIBABU YA KIBOBEZI cover image

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH ) Prof Abel Makubi amemtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), Ndugu David Kafulila na kushauriana maeneo ya miradi kadhaa ya uwekezaji inayotegemewa kuanzishwa na BMH ili kupanua au kuongezaΒ  huduma za kibobezi katika tiba na mahitaji ya chuo na mafunzo ya Afya.

Maeneo hayo ni pamoja na ujenzi wa Hostels za wanafunzi wa chuo, ndugu wa wagonjwa, wageni, vituo vya matibabu ya kibobezi vya kupandikiza Uloto, Upasuaji wa Moyo,Β  Ubongo, Taasisi ya tiba ya Macho, Maabara ya uchunguzi ya Genetics na kituo cha utafiti wa Tiba.Β 

Β