BMH KUONGEZA MASHIRIKIANO NA NMB

Published: Dec 10, 2025
BMH KUONGEZA MASHIRIKIANO NA NMB cover image
Menejimenti ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) itaendelea kukuza mashirikiano na Benki ya NMB katika kuboresha huduma za pande zote ili kuhakikisha Wananchi wengi wanafaidika na matunda ya uwekezaji wa Serikali yao.Β  Haya yamejiri katika kikao cha Mkurugenzi wa BMH Prof Abel Makubi alipokutana naΒ  Mkurugenzi MKuu Mtendaji wa NMB Bi. Ruth Zaipuna katika makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es SalaamΒ  na kukubaliana maeneo kadhaa ya kuongeza mashirikiano.
Β 
Prof. Makubi ametumia nafasi hiyo kuishukuru sana Menejimenti ya NMB kwa mchango kwa BMH katika kusaidia baadhi ya maboresho ya huduma yanayoendelea katika Hospitali hiyo .