Kliniki ya Magonjwa ya Dharula

Idara ya Tiba ya Dharura
Sifa za kipekee za idara (faida ya ushindani)
Idara ya Tiba ya Dharura ni rahisi kufikika, hasa wakati wa hali za dharura. Inafanya kazi saa 24 kila siku bila hitaji la miadi, hivyo kuwawezesha wagonjwa kupata huduma za matibabu wakati wowote wanapohitaji.
Huduma zinazotolewa na idara
· Huduma za uokoaji na uamsho (Resuscitation)
· Huduma za uangalizi wa muda (Observation services)
· Huduma kwa wagonjwa wa nje (Outpatient services)
· Huduma za maabara na famasia (Laboratory and pharmaceutical services)
Watoa huduma
· Madaktari Bingwa wa Tiba ya Dharura
· Wataalam wanaoendelea na mafunzo ya Tiba ya Dharura (Registrars)
· Wauguzi na wahudumu wa afya waliobobea katika tiba ya dharura
Idadi ya wagonjwa tunaowahudumia kwa mwaka
Takribani zaidi ya wagonjwa 60,000 kwa mwaka
Jinsi mgonjwa anavyoweza kufikia huduma zetu
Idara ya Tiba ya Dharura inatoa huduma saa 24 kila siku, hakuna haja ya kufanya miadi kabla ya kufika. Unakaribishwa wakati wowote unapohitaji huduma za dharura.
Taasisisi tunazoshirikiana nazo
ABOTT Fund Tanzania – Imesaidia kujenga kituo cha mafunzo kwa ajili ya ukanda wa kati ambapo kozi za msingi na za juu za Tiba ya Dharura hufundishwa.
Mikakati yetu ya kuboresha huduma
· Kufanya mafunzo ya mara kwa mara ndani ya hospitali kwa ajili ya kuboresha ujuzi wa wataalamu na kutoa huduma bora zaidi za tiba ya dharura.
Maboresho ya sasa
· Kuimarisha huduma za Emergency Medical Services (EMS) – Tunalenga kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma za gari la wagonjwa kwa urahisi na haraka wanapohitaji.
Kwa miadi ya kliniki na maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa namba:
📞 +255 (0) 735 000 002