Magonjwa ya Figo

Sifa za Idara (faida za ushindani)
Idara yetu inatoa huduma za wagonjwa wa nje na wa ndani kwa wagonjwa wenye magonjwa ya figo, pamoja na wagonjwa wenye kushindwa kwa figo wanaohitaji huduma za hemodialysis au upandikizaji figo.
Huduma zinazotolewa na idara
-
Kliniki ya Nefrolojia
-
Kliniki ya Upandikizaji Figo
-
Upandikizaji Figo
-
Hemodialysis
-
Huduma za wagonjwa wa ndani
Madaktari na watoa huduma wengine
Idara yetu ina madaktari bingwa 2 wa magonjwa ya figo (nephrologists), daktari bingwa 1 wa magonjwa ya ndani, daktari 1 wa tiba, wauguzi wa dialysis, wauguzi wa upandikizaji figo, na mtaalamu wa lishe.
Kliniki na huduma nyingine
-
Kliniki ya Nefrolojia
-
Kliniki ya Upandikizaji Figo
-
Upandikizaji Figo
-
Hemodialysis
-
Huduma za wagonjwa wa ndani
Idadi ya wagonjwa tunaowahudumia kwa mwaka
Tunatoa huduma za kliniki ya wagonjwa wa nje kwa zaidi ya wagonjwa 3,000 kwa mwaka, na pia tunafanya zaidi ya vipindi 10,000 vya hemodialysis kwa mwaka.
Mgonjwa anawezaje kupata huduma zetu?
Wagonjwa wanakaribishwa kufika katika idara yetu iliyopo Hospitali ya Benjamin Mkapa, ghorofa ya pili, jengo la Awamu ya Kwanza.
Taasisi tunazoshirikiana nazo na namna tunavyoshirikiana
-
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
-
Tokushukai Medical Group
-
Shonan Kamakura General Hospital
Tunashirikiana na taasisi hizi katika mafunzo, tafiti na maendeleo ya kitaaluma.
Mipango ya kuboresha huduma
Tunadhamiria kuboresha ubora wa huduma za afya tunazozitoa kwa wateja wetu kila siku.
Maboresho yanayoendelea sasa
Tunaendelea kuboresha huduma zetu kwa kupunguza muda wa kusubiri kliniki na kutoa huduma mapema kwa wagonjwa wapya.
Kwa ajili ya kuweka miadi ya kliniki au maswali zaidi, wasiliana nasi kupitia namba: +255 (0) 735 000 002.