Kliniki ya Upasuaji wa Neva

Idara ya Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu
Sifa za Idara (Faida za Ushindani)
- Inatoa huduma za wagonjwa wa nje (OPD) na wagonjwa wa kulazwa (IPD) wenye matatizo ya upasuaji wa mfumo wa neva
- Huduma bora, za kitaalamu, na zenye ufuatiliaji wa karibu
Huduma Zitolewazo na Idara
- Huduma za kliniki kwa wagonjwa wa nje
- Huduma kwa wagonjwa waliolazwa
- Upasuaji wa kitaalamu kwa matatizo ya mfumo wa neva
Madaktari na Watoa Huduma Wengine
Dkt. Henry Dotto Humba
- Daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu ya pembeni
- Hutoa huduma za tiba na upasuaji kwa matatizo yote ya mfumo wa neva
Kliniki na Huduma Nyingine
- Kliniki za wagonjwa wa nje hufanyika Jumatatu hadi Ijumaa
- Huduma hutolewa kwa wagonjwa wa rufaa na wanaofika moja kwa moja
Idadi ya Wagonjwa Tunaowahudumia kwa Mwaka
- Wagonjwa wa kliniki ya OPD: takribani 7200 kwa mwaka
- Upasuaji: takribani 427 kwa mwaka
Jinsi ya Kupata Huduma Zetu
- Huduma zote zinapatikana katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dodoma
- Wagonjwa wanaweza kufika moja kwa moja au kupitia mfumo wa rufaa kutoka hospitali nyingine
Taasisi Tunazoshirikiana Nazo na Namna ya Ushirikiano
- Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM): Mafunzo ya kitabibu kwa vitendo
- Tokushukai (Japan): Kuanzisha huduma za upasuaji wa mishipa ya fahamu (neurovascular) BMH — ikijumuisha mafunzo na vifaa
- MOI (Taasis ya Mifupa Muhimbili): Ushirikiano wa kitaalamu na huduma
- COSECSA: Mafunzo na usajili wa madaktari bingwa
Mipango ya Kuboresha Ubora wa Huduma
- Kutoa huduma bora kwa kila mteja katika kila hatua ya huduma
- Kufuata taratibu rasmi za utoaji huduma (SOPs) kwa usalama na ubora
Maboresho Yanayoendelea Kwa Sasa
- Kuongeza idadi ya madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mgongo
- Kupata vifaa vya kisasa vya kusaidia upasuaji wa hali ya juu
- Kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kusaidia upasuaji (support staff)
Kwa Kuhifadhi Nafasi ya Kliniki au Maswali Zaidi
Wasiliana nasi kupitia:
📞 +255 (0) 735 000 002