Mwanzo / Development Projects / Idara ya Kansa na Mionzi

Idara ya Kansa na Mionzi

02 Oct, 2024
Idara ya Kansa na Mionzi

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) inaendelea kuonesha dhamira yake ya dhati ya kuboresha huduma za afya kupitia utekelezaji wa miradi muhimu ya miundombinu. Maendeleo haya yanayondelea yanalenga kupanua utoaji wa huduma, kuhakikisha viwango vya juu vya huduma bora, na kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wagonjwa kutoka Dodoma na maeneo mengine nchini.

Moja ya miradi mikubwa inayoendelea kwa sasa ni ukamilishaji wa vyumba vitatu vipya vya upasuaji, ambavyo vitaongeza uwezo wa upasuaji na kupunguza muda wa kusubiri kwa wagonjwa. Sambamba na uongozi wake katika huduma za figo, hospitali pia inakamilisha upanuzi wa kitengo cha Upandikizaji Figo, ili kuhakikisha wagonjwa wengi zaidi wanapata huduma hii ya uokoaji maisha hapa nchini.

Ili kusaidia matibabu ya kitaalamu, ujenzi wa Kituo cha Matibabu ya Saratani unaendelea kwa kasi. Mara utakapokamilika, kituo hiki kitatoa huduma za tiba ya saratani kwa ukamilifu, hivyo kupunguza mahitaji ya wagonjwa kusafiri kwenda vituo vya mbali.

BMH pia inapa kipaumbele eneo la elimu na mafunzo ya vitendo kupitia ujenzi wa Maabara ya Mafunzo ya Dharura (EMD Lab Skills Center) na Maabara ya Mafunzo ya Upasuaji (Surgical Lab Skills Center), zitakazowezesha wataalamu wa afya kujifunza kwa vitendo. Vilevile, hospitali inapanga kuanzisha huduma za uchunguzi wa afya wa kisasa, ikiwemo eneo maalum kwa ajili ya Master Check-up na Fast Track Clinics kwa ajili ya kuhudumia wateja kwa haraka na kwa ufanisi.

Miundombinu ya kusaidia huduma muhimu pia haijasahaulika. Hospitali inakarabati mifumo ya oksijeni, vifaa vya kiyoyozi, majenereta, na miundombinu ya maji ili kuhakikisha huduma zinaendelea bila usumbufu na kuongeza faraja kwa wagonjwa. Kazi za ukarabati pia zinaendelea katika maeneo ya utoaji dawa, Idara ya Macho, pamoja na ofisi za utawala.

Katika juhudi zake za kuhudumia wagonjwa kwa ubora na hadhi, BMH inaongeza idadi ya vyumba vya VIP/binafsi, kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji faragha na huduma za kibinafsi. Aidha, hospitali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha Mpango Kabambe wa Maendeleo (Master Plan), utakaoongoza mwelekeo wa muda mrefu wa upanuzi wa hospitali.

Miradi hii yote ya miundombinu inaakisi dira ya BMH ya kuwa kitovu cha umahiri katika utoaji wa huduma za afya, siyo tu kwa Tanzania bali kwa ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati. Kwa kila mradi unaokamilika, hospitali inachukua hatua moja zaidi kuelekea kutoa huduma salama, za kisasa, na zinazomlenga mgonjwa kwa kiwango cha kimataifa.


Tofauti Kati ya Radiotherapy na Nuclear Medicine

Radiotherapy (Tiba kwa Mionzi)

  • Lengo: Kutibu saratani kwa kuharibu au kuzuia ukuaji wa seli za saratani.
  • Jinsi Inavyofanya Kazi: Inatumia mionzi ya hali ya juu kama X-ray, gamma rays, au chembe zenye chaji kuharibu DNA ya seli za saratani.
  • Aina:

ü  External Beam Radiation Therapy (EBRT) – mionzi kutoka nje ya mwili.

ü  Brachytherapy – mionzi huwekwa ndani au karibu na uvimbe.

ü  Systemic Radiation Therapy – mionzi huingizwa kwa njia ya kumeza au sindano ili kufikia seli za saratani ndani ya mwili.

  • Matumizi: Tiba ya saratani (kuponya au kupunguza maumivu) kwa kushirikiana na upasuaji au kemikali (chemotherapy).

Nuclear Medicine (Tiba na Uchunguzi kwa Mionzi ya Nyuklia)

  • Lengo: Kwa uchunguzi (diagnosis) na pia matibabu ya magonjwa mbalimbali kama saratani, magonjwa ya moyo, na mfumo wa neva.
  • Jinsi Inavyofanya Kazi: Inatumia kiasi kidogo cha mionzi (radiopharmaceuticals) kuingizwa mwilini kwa sindano, kumezwa au kuvutwa. Kisha kamera maalum hupiga picha za viungo kwa kutumia mionzi hiyo.
  • Aina:

ü  SPECT (Single Photon Emission Computed Tomography)

ü  PET (Positron Emission Tomography)

ü  Matibabu kwa kutumia mionzi maalum kama Iodine-131 au Lutetium-177.

  • Matumizi:

ü  Uchunguzi: Kuona mtiririko wa damu, kubaini uvimbe, na kutathmini kazi za viungo.

ü  Matibabu: Tiba kwa saratani fulani (kwa mfano ya tezi) au magonjwa sugu ya tezi.

Kwa pamoja, Radiotherapy na Nuclear Medicine ni nyanja mbili muhimu zinazosaidia kugundua na kutibu magonjwa kwa kutumia teknolojia ya mionzi kwa usalama na ufanisi mkubwa.

                                              WhatsApp Image 2025-07-01 at 22.03.49 (1).jpeg

                                                                     Ujenzi wa Kituo cha Mionzi kwa Matibabu ya Saratani BMH

 

Hospitali inatoa wito wa kusaidia au uwekezaji wa pamoja katika Miradi ifuatayo;
 1. Ujenzi wa Kituo Bora cha Afrika Mashariki katika Upandikizaji Uloto, 
 2. Upandikizaji Figo, 
 3. Upandikizaji Ini, 
 4. Taasisi ya Moyo na Mishipa,
 5. Taasisi za Macho na ENT na Kituo cha Neuroscience.
 6. Usambazaji wa bidhaa za Afya Kuanzisha Kituo cha Maabara ya Molekuli na Vinasaba 
 7. Kuanzisha Benki ya seli Ujenzi wa Kituo cha Utafiti wa Majaribio ya dawa tiba 
 8. Ujenzi wa Nyumba za Watumishi 
 9.  Ujenzi wa Hosteli 
10. Wanafunzi wa Udaktari Ujenzi wa Hosteli kwa Ndugu wa Wagonjwa
11. Kuipatia Hospitali Mashine ya Teknolojia ya Juu inayotumika AI Upasuaji wa roboti 
12. Usanifu na ujenzi wa Jiji la Utalii wa Matibabu ndani