Mwanzo / Huduma Zetu / Hospitali ya Benjamin Mkapa imejipanga kutekeleza dira ya taifa 2025 - 2050

Hospitali ya Benjamin Mkapa imejipanga kutekeleza dira ya taifa 2025 - 2050

Published on July 17, 2025

Article cover image

Na. Jeremiah Mbwambo,17/07/2025, Gitega-Burundi 

Mkurugenzi Mtendaji Prof. Abel Makubi ameeleza kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) tumeanza kuitekeleza Dira hiyo na ndiyo maana watalaamu wapo leo hapa Burundi kutoa hayo Matibabu kama sehemu ya Tiba Utalii.

"Tumejipanga kuitekeleza Dira hii iliyo zinduliwa leo kwakuwa imegusa sekta ya afya katika mwelekeo(ustawi wa jamii) , katika malengo , nguzo  na matarajio katika azima ya kuwa na Taifa lenye Jamii yenye Afya bora . Serikali kupitia BMH tayari inaendelea  kuwekeza kuwa kituo cha kuvutia utalii wa matibabu ya ubingwa na ubobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa” alisema Prof.  Makubi 

Ameongeza kuwa BMH inaendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma za matibabu 

"Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) tunaendelea kufanya tafiti ambazo zinaendelea kuimarisha huduma tunazozitoa na ndani ya miaka 25 ijayo maono yetu ni eneo la BMH na UDOM kuwa sehemu ya Dodoma Medical Tourism City; amesema  Prof. Makubi 

Aidha ameshukuru Dira kuliwekea mkazo suala la upatikanaji madawa na vifaa tiba ambapo sasa tukawekeza katika viwanda vyetu vitakavyo zalisha vifaa tiba na vitendanishi 

"Hivi karibuni tumeshuhudia Waziri wa Afya wakiingia hati yamakubaliano na shirika moja ambalo litaanza kuzalisha vifaa tiba Tanzania, hii ni hatua ya kupongezwa na inatakiwa kuendelezwa ili tupate mashirika mengi zaidi ya uzalishaji wa vifaa tiba na vitendanishi" alisema Prof. Makubi 

Hospitali ya Benjamin Mkapa imewekezwa kwa vifaa tiba kisasa na madaktari Bingwa hali inayopelekea kupeleka huduma nje ya dodoma na nje ya Tanzanian kutokana na uwekezaji wake na hivi sasa kuna timu ya madaktari Bingwa wapo Burundi kutoa huduma.