WANANCHI 2420 WA BURUNDI WANUFAIKA NA MATIBABU YA UBINGWA WA MADAKTARI WA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA.
Na. Jeremiah Mbwambo, Bujumbura - Burundi, 26/07/2025
Mratibu wa kambi ya matibabu na Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Bi. Monica Kessy amesema mwitikio wa kupokea matibabu haya umekuwa mkubwa
"Kwasiku 10 tulizokuwa hapa Burundi tumeona wananchi 2420, ambapo kati yao wagonjwa 125 wamefanyiwa upasuaji wote walio fanyiwa upasuaji wanaendelea vizuri na wengi wamesha ruhusiwa kwenda nyumbani" amesema Bi. Monicaย
Ameongeza kuwa kambi hii imetoa fursa kwa wananchi wa Burundi ambao matibabu yameshindikana hapa tumewapa rufaa ya kwenda Hospitali ya Benjamin Mkapaย
"Serikali ya Tanzania imewekeza vifaa tiba vya kisasa ambavyo vinawezesha kufanya uchunguzi kwa kina na kutoa matibabu sahihi hivyo wagonjwa 67 tumewapa rufaa ya kwenda Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma" amesema Bi. Monicaย
Mafanikio ya kambi hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta ya afya ususani katika Hospitali ya Benjamin Mkapa katika kusomesha madaktari na kununua vifaa tiba hali inayo pelekea Hospitali hiyo kuwa na uwezo wa kufanya utalii wa matibabu.