HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA NA INTERBURNS YA UINGEREZA WAKUBALIANA KUBORESHA HUDUMA ZA MATIBABU YA MAJERAHA YA MOTO
Na. Jeremiah Mbwambo
Picha na Jeremia Mwakyoma
Oktoba 28, 2025
Hati ya makubaliano hayo imesainiwa jijini Dodoma katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, hati hiyo ya makubaliano imelenga kuanzisha kitengo na wodi maalumu ya wagonjwa wenye majeraha yatokanayo na kuungua moto
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof. Abel Makubi amewahakikishia Interburns kusimamia makubaliano hayo
"Niwahakikishie tutasimamia makubaliano haya tunayo ingia leo kwa kuwa ni sehemu ya kuboresha huduma zetu ambazo ni maslahi ya mgonjwa anaye fika hospitalini hapa, na kujengeana uwezo katika mafunzo, miundombinu, vifaa na tafiti” amesema Prof. Makubi
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Interburns Society Bi. Tina Bajec ameeleza dhamira ya kushirikiana
"tumejitolea kuwasaidia watanzania hususani kupitia Hospitali na leo tunaingia tunasaini hati ya makubaliano ili kutuwezesha kufikia malengo ya kutoa msaada" amesema Bi. Tina
Kwa upande wake Mkuu wa Idara Dkt. Samwel Wambura amesema makubaliano haya yatatoa msaada mkubwa kwa wagonjwa wa moto
"Makubaliano haya tuliyo ingia leo yatatoa msaada wa kuanzisha kitengo na wodi maalumu ya wagonjwa walioungua, matibabu yatatolewa kwa kina na vifaa tiba" amesema Dkt. Wambura
Wakati Hospitali ya Benjamin Mkapa ikiwa inaadhimisha miaka kumi huku ikiendelea kuongeza wigo wa mashirikiano ya kitaifa na kimataifa