HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YA ANZA MATIBABU YA KUONDOA MAUMIVU SUGU YA MGONGO BILA KUFANYA UPASUAJI (FACET INJECTIS AND EPIDURAL BLOCK )

Published: Nov 19, 2025
HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YA ANZA MATIBABU YA KUONDOA MAUMIVU SUGU YA MGONGO BILA KUFANYA UPASUAJI (FACET INJECTIS AND EPIDURAL BLOCK ) cover image

Na. Jeremiah Mbwambo, Dodoma, 19/11/2025

Daktari Bingwa wa Ubongo na mishipa ya fahamu Hospitali ya Benjamin Mkapa Maxgama Ndosi ameeleza kuwa matibabu haya ni ya ubingwa wa juu

"Leo tumeanzisha matibabu haya na tunafanya sisi wenyewe kwamaana ya madaktari Bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, tumefanikiwa kumuhudumia mgonjwa wa kwanza na ametoka salama, matibabu haya yanahusisha sindano maalumu katika uti wa mgongo mgonjwa akishapata matibabu haya maumivu ya mgongo yanaondoka kabisa" amesema Dkt. Ndosi

Ameongeza pia matibabu haya yanaondoa adha ya mgonjwa kukaa wodini

"Matibabu haya ya namuondolea adha mgonjwa kukaa wodini kwa kuwa hayausishi upasuaji, hivyo anapopatiwa matibabu haya anaondoka siku hiyo hiyo "amesema Dkt. Ndosi

Kwa upande wa mgonjwa (jina limeifadhiwa) ameeleza baada ya kupata matibabu hayo

"Nilikuwa namaumivu makali sana ya mgongo ilikuwa inanipelekea kushindwa kutembea au kuinua vitu lakini baada ya kupata matibabu haya nilipo maliza kuchoma sindano hapo hapo sikusikia maumivu mpaka sasa sina maumivu" amesema Mgonjwa

Hospitali ya Benjamin Mkapa inakuwa ni yapili kutoa matibabu haya nchini na niyakwanza kwa ukanda wa kati, wakati Hospitali ya Benjamin Mkapa ikiadhimisha miaka kumi tangia ianze kutoa huduma imeendelea kuongeza huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa wa juu