HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA (BMH) YAHITIMISHA KAMBI YA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA UBINGWA BOBEZI WILAYANI IRAMBA MKOANI SINGIDA, WANANCHI 450 WANUFAIKA

Published: Mar 03, 2026
HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA (BMH) YAHITIMISHA KAMBI YA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA UBINGWA BOBEZI WILAYANI IRAMBA MKOANI SINGIDA, WANANCHI 450 WANUFAIKA cover image
Na Jeremia Mwakyoma
SINGIDA - FEB 27, 2026 
 
 
 
Akizungumza wakati wa kuhitimisha kambi hiyo, Mratibu wa Kambi Dkt. Emiliana Myovela amesema kuwa kati ya Wananchi hao 450 waliopata huduma, Wananchi 28 wamefanyiwa upasuaji na wengine wamepewa rufaa ya kwenda BMH Dodoma. 
 
 
 
"Wagonjwa 88 tumewapa Rufaa ya kwenda BMH kutokana na hali zao kuhitaji uchunguzi zaidi, matibabu zaidi ya kibobezi na upasuaji, lakini kwa ujumla wananchi wamekuwa na mwitikio chanya, kambi hii imetumika kuwajengea uwezo Watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba" alisisitiza Dkt. Myovela. 
 
 
 
Akitoa salamu za Serikali ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Suleiman Mwenda ameishukuru BMH kwa kupeleka huduma Wilayani humo; amesema pamoja na huduma za Afya zinazopelekwa Ngazi ya Vijiji na Kata na Wilaya, bado maeneo hayo yanahitaji huduma za Kibingwa na Kibobezi, kupitia kambi za matibabu inasaidia kufikisha huduma hizo. 
 
 
 
"Kwa sasa uelewa na mwamko wa Wananchi kufika kwenye vituo vya Afya na Hospitali kupata huduma za kitaalamu umekuwa mkubwa na Serikali pia inawekeza sana kwenye huduma za Afya" alifafanua zaidi Mhe Mwenda.