HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA TAASISI YA AFYA CHECK FOUNDATION

Published: Jan 05, 2026
HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA TAASISI YA AFYA CHECK FOUNDATION cover image

Na Jeremia Mwakyoma

DODOMA - JANUARI 5, 2026

 

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) na Taasisi ya Afya Cheki Foundation Leo zimeingia rasmi makubaliano ya kushirikiana. 

 

Akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini hati ya makubaliano (MoU) baina ya Taasisi hizo mbili, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Dkt. Henry Humba ametaja maeneo ya mashirikiano yakijumuisha kutangaza Huduma za Tiba Utalii zinazotolewa na BMH, Utoaji wa Huduma Mkoba (Outreach Services) na utafutaji wa rasilimali fedha kupitia wadau mbalimbali ili kugharamia huduma za Afya kwa wananchi wenye uhitaji.

 

 

"Makubaliano tuliyosaini leo na wenzetu wa Afya Check Foundation yatasaidia katika kupromote tiba utalii, uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika Sekta ya Afya unatoa fursa ya kutumia huduma za Afya katika utalii, kwa kutangaza huduma za Afya zinazotolewa na BMH hususani maeneo ambayo BMH haijaweza kufika katika nchi mbalimbali na kuvutia Wananchi kutoka mataifa hayo kuja kutibiwa Tanzania hapa BMH" alisisitiza Dkt. Humba.

 

 

Dkt. Humba aliongeza kuwa eneo jingine ambalo BMH inatarajia kushirikiana na Taasisi hiyo ni kuimarisha Huduma Mkoba hapa ndani ya nchi na katika nchi mbalimbali kwa kupeleka kambi za matibabu ya Kibingwa na Kibingwa Bobezi kwenye nchi mbalimbali kwa kuzingatia Taasisi ya Afya Check Foundation ina uzoefu wa kutosha wa muda mrefu katika eneo hilo.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya Check Foundation Dkt. Isaac Maro amesema taasisi yake inauzoefu wa kutosha wa muda mrefu katika shughuli za "kupromote" masuala ya Afya tangu mwaka 2009 na kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na BMH wameona ni jambo la muhimu elimu na taarifa hizo kuwafikia Watanzania wengi na Mataifa mengine nje ya Tanzania. 

 

"Tunakuja kushirikiana na BMH kuongeza nguvu kwenye programu za kutafuta rasilimali fedha ili kuweza kuwafikishia huduma Watanzania wengi zaidi wenye uhitaji, wasio na uwezo; tutapromote na kuweka campaign za kupata fedha kupitia Wadau ambao wana fedha na wako tayari kusuport huduma za Afya kwa ajili ya kusaidia Wananchi" alibainisha Dkt. Maro

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

BENJAMIN MKAPA HOSPITAL SIGNS COLLABORATION AGREEMENT WITH AFYA CHECK FOUNDATION

 

By Jeremia Mwakyoma  

DODOMA – JANUARY 5, 2026

 

Benjamin Mkapa Hospital (BMH) and Afya Check Foundation have officially entered into a partnership agreement today.

 

Speaking during the signing ceremony of the Memorandum of Understanding (MoU) between the two institutions, Acting Executive Director of BMH, Dr. Henry Humba, highlighted areas of collaboration including promoting medical tourism services offered by BMH, outreach services, and mobilizing financial resources from various stakeholders to support healthcare services for underserved communities.

 

"The agreement signed today with our partners from Afya Check Foundation will help promote medical tourism. The major investments made by the Government in the Health Sector provide an opportunity to market health services offered by BMH, especially in areas the hospital has not yet reached internationally, and attract patients from other countries to seek treatment here at BMH in Tanzania," emphasized Dr. Humba.

 

He further added that another key area of collaboration will be strengthening outreach services both within the country and abroad by organizing specialist and super-specialist medical camps, leveraging the long-standing experience of Afya Check Foundation in this field.

 

On his part, Dr. Isaac Maro, Director of Afya Check Foundation, said the foundation has long-standing experience in promoting health issues since 2009. Recognizing the great work being done by BMH, they saw the importance of ensuring that information and education reach more Tanzanians and international communities.

 

"We aim to collaborate with BMH to boost fundraising programs so we can reach more Tanzanians in need those without the means. We will promote and run campaigns to raise funds from stakeholders who are willing to support health services for the benefit of the people," explained Dr. Maro.