Mwanzo / Huduma Zetu / Hospitali ya Benjamin Mkapa Kuzindua Huduma Mpya za "Royal, International Patients and Master Health Check Up Clinic.

Hospitali ya Benjamin Mkapa Kuzindua Huduma Mpya za "Royal, International Patients and Master Health Check Up Clinic.

Published on July 08, 2025

Article cover image

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) inatarajia kuzindua huduma maalum na za kibunifu zijulikanazo kama “Royal, International Patients and Master Health Check-Up Clinic.” Huduma hizi zinalenga kutoa huduma bora, ya haraka na ya kipekee kwa viongozi, watu mashuhuri, watalii wa afya kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na wananchi wanaohitaji uchunguzi wa kina wa afya kwa wakati mmoja.

Kliniki hii maalum itatoa huduma zenye viwango vya kimataifa kwa kutumia teknolojia ya kisasa, mazingira ya faragha, na wataalamu waliobobea kutoka idara mbalimbali. Kupitia huduma ya “Master Health Check-Up,” wagonjwa wataweza kufanyiwa uchunguzi wa kina wa afya kwa siku moja (one-day comprehensive health screening), kwa ajili ya utambuzi wa mapema wa magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, saratani, matatizo ya ini, figo, mapafu na mengineyo.

Kwa upande mwingine, huduma za “Royal and International Patients Clinic” zitahakikisha ufuatiliaji maalum, uratibu wa haraka wa vipimo, uangalizi wa karibu na mawasiliano ya moja kwa moja kati ya madaktari na mgonjwa. Huduma hizi zitakuwa na mazingira maalum ya mapokezi, vyumba vya kusubiri vya daraja la juu, pamoja na ratiba zilizopangwa kulingana na mahitaji ya mteja.

Kupitia mpango huu, BMH inalenga kuvutia watalii wa afya kutoka mataifa jirani na ya mbali, kukuza hadhi ya hospitali kitaifa na kimataifa, na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya afya nchini Tanzania.

Huduma hizi mpya ni sehemu ya mkakati wa hospitali wa kupanua huduma za kibingwa na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa kila mtu – bila kujali mipaka.

Hivyo Unakaribishwa katika sikuya uzinduzi wa huduma hizi maalaumu kwa ajili yako.