BMH NA RADBOUD-UMC KUJENGA UWEZO WA MABINGWA BOBEZI

Published: Aug 28, 2026
BMH NA RADBOUD-UMC KUJENGA UWEZO WA MABINGWA BOBEZI cover image

28 August 2026, Nijmegen, Uholanzi.

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imeanza mashirikiano na Radboud University Medical Center (RMUC) ya nchini Uholanzi ili kuwezesha mpango wa kuongezea ujuzi watalaamu katika maeneo mbalimbali ya ubingwa bobezi wa matibabu.

Hatua hiyo imefikiwa katika ziara ya Watalamu wa BMH ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Prof. Abel Makubi katika taasisi hiyo ya RMUC.

Maeneo ya kuongeza ujuzi ni pamoja na ubingwa wa upasuaji wa koo, masikio, na pua(ENT) magonjwa ya kuambukiza (Infectious diseases) , huduma za uzazi saidizi(IVF), Saratani , huduma za usingizi na mahututi, Uuguzi katika huduma za kibobezi, Tibalishe, Tafiti za magonjwa , kambi za Matibabu na kubadilishana ujuzi wa Watalaamu na Wanafunzi katika Mafunzo.