BMH YASOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA.
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) inashiriki maonesho ya wakulima nanenane ikiwa ni sehemu ya kufahamisha umma kuhusu huduma zinazotolewa na kusogeza huduma karibu na jamii.
Sambamba na maonesho hayo BMH inatoa huduma za magonjwa ya moyo, magonjwa ya macho, vipimo vya maambukizi ya ukimwi, vipimo vya kisukari pamoja na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa madaktari bingwa.
Maonesho hayo ni ya siku nane kuanzia Agosti 1 hadi Agosti 8, 2025.