BMH DAY OCT. 13, 2026: MIAKA 10 IJAYO HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUWA HOSPITALI BORA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Published: Oct 29, 2026
BMH DAY OCT. 13, 2026: MIAKA 10 IJAYO HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUWA HOSPITALI BORA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI NA KATI cover image

Na Jeremia Mwakyoma, Gladys Lukindo
Picha na Jeremiah Mbwambo
DODOMA - OKTOBA 13, 2026

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Prof. Abel Makubi kwa Watumishi wote wa BMH wakati wa hafla ya jioni ya kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Oktoba 13, 2015 inayojulikana kama "OKTOBA 13, hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

"Watumishi wote wa BMH naomba tutambue kuwa katika kipindi hiki cha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Hospitali yetu, tumefanikiwa kutoa huduma bora na kukuza hadhi ya Hospitali yetu na hivi karibuni  tunaelekea kupata hadhi ya kuwa  Hospitali ya Taifa, kazi na malengo yaliyopo mbele yetu kila mmoja atambue kuwa BMH imepanga kuwa Hospitali inayoongoza kwa ubora wa huduma kwa ukanda wote wa Afrika Mashariki" alisisitiza Prof. Makubi

WhatsApp Image 2026-10-29 at 6.28.10 PM.jpeg

Aliongeza kwa kuwataka watumishi kuongeza moyo wa kuwatumikia wananchi, moyo wa ushirikiano na kutambua kuwa BMH ndio mama wa watumishi wote waliopo BMH hivyo wana wajibu wa  kuipambania kwa hali na mali kwa matarajio kuwa kasi hiyo ikiendelea BMH inakwenda kuwa Hospitali inayoongoza kwa ubora kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.

Prof. Makubi alitumia hafla hiyo kuwapongeza watumishi wote wa BMH kwa utoaji wa huduma bora na kukabidhi Tuzo ambayo BMH imeshinda nafasi ya Mshindi wa Tatu miongoni mwa Mashirika yote  308 ya Umma zilizotolewa na Msajili wa Hazina jijini Arusha wakati wa Mkutano wa Watendaji wakuu na Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya umma, huku akiwatqka watumishi hao kuendeleza utamaduni huo wa kutoa huduma zenye viwango vya juu vya ubora.

WhatsApp Image 2026-10-29 at 6.29.55 PM.jpeg

Nae Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa BMH Bw. Mathias Mhembe  katika sherehe hiyo ameelezea kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye sekta ya Afya kiasi cha kuiwezesha BMH kuwa Hospitali inayotoa huduma za Kibingwa Bobezi na kuvutia wananchi kutoka kanda mbalimbali nchini na nchi zinazotuzunguka.

 

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa Uongozi wa BMH kutoa tuzo kwa Mtumishi Bora wa mwaka 2026 wa Hospitalinya BMH Sr. Joyce Ndosi ambaye ni msimamizi wa Kliniki ya Wateja Maalumu, wa Kimataifa na uchunguzi wa Afya wa Kina (Royal, International Patients and Master Health Check up).