BMH YAIBUKA NA USHINDI WA VIKOMBE VITATU SHIMMUTA 2025

Published: Dec 10, 2025
BMH YAIBUKA NA USHINDI WA VIKOMBE VITATU SHIMMUTA 2025 cover image
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imeibuka kinara baada ya kujinyakulia jumla ya vikombe vitatu katika mashindano ya SHIMMUTA yaliyomalizika leo mkoani Morogoro.
 
Katika mashindano hayo, timu ya BMH ilitwaa nafasi ya kwanza kwenye mchezo wa Pool table na Karata, pamoja na nafasi ya tatu kwenye mchezo wa Bao.
 
Ushindi huo umechagizwa na maandalizi madhubuti, nidhamu ya hali ya juu, na mshikamano miongoni mwa wanamichezo wa BMH. 
 
Mashindano ya SHIMMUTA yalianza Novemba 25 na kukamilika Desemba 6, 2025, yakibeba kaulimbiu: “Uongozi Imara kwa Michezo Endelevu: Michezo ni Daraja la Afya, Amani, Umoja, na Mshikamano wa Kitaifa.”