Mwanzo / Huduma Zetu / BMH YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI - SINGIDA

BMH YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI - SINGIDA

Published on May 02, 2025

Article cover image

Watumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) leo wameungana na wafanyakazi wengine kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Singida.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni, Dkt. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maadhimisho hayo huadhimishwa May 1 kila mwaka kwa kuwakutanisha  kwa pamoja wafanyakazi wa sekta binafsi na umma. 

Maadhimisho hayo yamebeba Kauli mbiu isemayo Kauli Mbiu ya Mei Mosi: Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi sote Tushiriki