BMH YAPOKEA MADAKTARI BINGWA KUTOKA MAREKANI KWA AJILI YA KAMBI MAALUMU YA MATIBABU YA MACHO

Published: Mar 09, 2026
BMH YAPOKEA MADAKTARI BINGWA KUTOKA MAREKANI KWA AJILI YA KAMBI MAALUMU YA MATIBABU YA MACHO cover image

Na Jeremia Mbwambo

DODOMA – MACHI 9, 2026

 

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Prof Abel Makubi, leo amewapokea madaktari na wataalam wa Moran Eye Centre, ambacho ni kituo cha Macho katika Chuo Kikuu cha jimbo la Utah, Marekani

 

"Ninawashukuru kwa kuja kutusaidia kutujengea uwezo kwa watumishi wetu. BMH inauhitaji wa kuongeza huduma  za macho pamoja na jengo linalo jitegemea la utoaji wa huduma hizo, ninawaalika Morani na wadau wengine mnao weza kuja kutuunga mkono katika kufikia haya" amesema Prof. Makubi

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Global Eye Services at Moran ya Chuo Kikuu cha Utah Marekani Lori McCoy, ameeleza furaha yake ya kufanya kazi na BMH

 

"Tunafuraha kuwa sehemu ya mashirikiano na ninyi na tunapo badilishana uzoefu pamoja na wataalamu wa hapa, inaleta manufaa kwa wananchi wa Tanzania kila tunapokuja tunaona jinsi mlivyokuwa na mnavyo endelea katika utoaji wa huduma za macho" amesema McCoy

 

Hata hivyo Daktari Bingwa wa Macho Frank Sandi amesema idadi ya watu watakao fanyiwa upasuaji wa macho ni idadi kubwa lakini watafanyiwa wote.

 

"Tulianza uchunguzi tarehe 23 mwezi wa pili kwa wiki 2 mpaka tarehe 6 Mwezi wa tatu 2026, kwa kipindi hicho tumechunguza wagonjwa 1250 na kupata wanaotakiwa kufanyiwa matibabu ya upasuaji BMH ni 280" amesema Dkt. Frank

 

BMH kwa kushirikiana na Moran wanafanya kambi kuanzia leo mpaka tarehe 13/03/2026