BMH WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA UFATILIAJI NA TATHMINI
Na Gladys Nicodemus Lukindo, Dodoma
Watumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wapewa mafunzo ya mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ili kuboresha utendaji kazi.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Ufatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Afya, Bw. Claud Kumalija amesema mfumo huu utasaidia kuleta ufanisi katika kazi.
“ Lengo la mfumo huu ni kupima matokeo na ufanisi wa utendaji kazi ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi, hivyo niwaombe mtumie mafunzo haya kuelewa mfumo ili kuwa na ufanisi katika kazi, “ amesema Bw. Kumalija.
Aidha, Bw. Kumalija ameongeza kuwa mfumo huu ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kuongeza uwajibikaji kwa watumishi na ufanisi wa utendaji kazi .
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dkt. Abdallah Baja amewataka watumshi kutumia muda wa mafunzo vizuri ili kuleta matokeo mazuri katika utendaji kazi.
“Niwaombe mtumie muda huu vizuri katika kujifunza na kupata uelewa wa huu mfumo ili kuleta matokeo chanya katika kuboresha na kutoa huduma bora kwa wananchi,” amesema Dkt. Baja.
Mbaraka Hassan, mshiriki wa mafunzo ya ufatiliaji na Tathmini wa BMH amesema mafunzo haya yatasaidia taasisi katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi , na kuwafanya watumishi kuwajibika katika majukumu yao na kusidia kutimiza malengo ya Taasisi na wizara katika kupeleke kutimiza dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050.