BMH KUPANUA UBOBEZI WA MATIBABU YA MOYO KWA KUSHIRIKIANA NA HOSITALI ZA UHOLANZI NA UJERUMANI.
Uholanzi/Ujerumani, 28 August 2026.
Katika kuimarisha Diplomasia ya Afya na kuboresha ujuzi wa watalaamu ngazi ya ubobezi, Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imekubaliana na Hospitali za Amphia (Breda) na Schuechtermann-klinik (Heart Center-Bad Rotherfelde, Ujerumani) kuweka Road Map ya kupanua zaidi huduma za kibobezi za Moyo katika taasisi ya BMH .
Mpango huu umefikiwa katika ziara ya Watalaamu wa BMH na Viongozi wa Amphia Hospital na Schuechtermann-klinik chini ya uratibu wa ZGT Overzee ya Uholanzi.
Chini ya Road Map hii ya miaka mitano BMH itaweza kusaidiwa mafunzo ya matibabu ya juu kwa Watalaamu wake , ndani na nje ya Tanzania. BMH pia itaendelea kushirikiana na taasisi za ndani kama JKCI, KCMC, BMC na Aghakan ili kutumia vizuri watalaamu waliopo katika kuimarisha huduma hizo. Mashirikiano kati ya BMH na taasisi za ndani na za nje ya nchi ni moja ya vipaumbele vya BMH katika kujenga kituo bora cha Matibabu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.