BMH KUTOA HUDUMA KATIKA MKUTANO WA RUWASA NA CBWSOs
Na Ludovick Kazoka na Gladys Lukindo, Dodoma: February 27, 2026
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) inashiriki mkutano wa Wakala wa Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ulioanza leo katika jengo la NMB Mtumba mji wa Serikali.
Lengo la kushiriki kwa BMH katika tukio hilo la siku mbili ni kutoa huduma ya dharura ya vipimo na matibabu kwa washiriki.
Ndugu Samuel Makassy, mmoja wa washiriki, amesema amenufaika kwa kupima ugonjwa wa kisukari na blood pressure.
"Naishukuru Hospitali kwa kuleta huduma hizi hapa kwenye hili tukio, nimepata fursa pia ya elimu ya afya," amesema Ndg Makassy, ambaye ni mkazi wa Nkuhungu, Dodoma.
Ndugu Ruben Setabahu, mkazi wa Mtumba, amesema anashukuru kwa vipimo alivyopata na kwamba ataenda BMH kwa vipimo zaidi.
" Nawashukuru wataalamu wamenifanyia vipimo vya shinikizo la damu, nimeshauriwa kwenda Hospitali kwa vipimo zaidi na matibabu,
Kwa mujibu wa Dkt, Faith Mapanje, kutoka Idara ya Magonjwa ya Dharura, amesema BMH inatoa huduma za dharura na vipimo vya shinikizo la damu na kisukari.
Mkutano huo umeambatana na maonyesho ya huduma za maji ambapo BMH inatoa huduma kwa washiriki na wananchi waliokuja kuona huduma za maji.