BMH , UDOM NA TOKUSHUKAI -JAPAN kukamilisha taratibu za msaada wa tzs 28 billion wa ajili ya kituo cha umahiri cha upandikizaji figo

Published: Oct 24, 2025
BMH , UDOM  NA TOKUSHUKAI -JAPAN kukamilisha taratibu za msaada wa tzs 28 billion wa ajili ya kituo cha umahiri cha upandikizaji figo cover image

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Prof. Abel Makubi ameuaga ujumbe wa Tokushikai toka Japan na kukubaliana kukamilisha taratibu zote za msaada wa TZS Billion 28 kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha Umahiri cha Tiba , Mafunzo na Utafiti wa Upandikizaji Figo .


"Ninawashukuru kwa kujitoa kwenu na kuamua kuleta msaada huu mkubwa wa ujenzi wa jengo la matibabu ya upandikizaji figo, tufikishieni salamu kwa mwenyekiti wa Tokushikai" amesema Prof.  Makubi


Ujumbe huo umefika BMH na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuleta taarifa ya ujio wa mwenyekiti wa Tokushikai kuja kusaini mkataba wa ujenzi wa jengo la upandikizaji figo mnamo mapema mwezi disemba 2025, aidha ujumbe huo umehakiki maeneo yote yaliyo pendekezwa kurekebishwa katika mkataba wa msaada, kabla ya kusainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na TOKUSHUKAI-Japan . Ujumbe huo pia ulipata nafasi ya kukutana na Uongozi wa UDOM, Wizara ya Fedha, Afya, na Taasisi zingine za Serikali ili kukamilisha taratibu zinazohitajika kabla ya Disemba 2025.