Mwanzo / Huduma Zetu / BMH , UDOM  na TOKUSHUKAI JAPAN WASAINI MAKUBALIANO YA KUANZA UJENZI WA KITUO CHA UMAHIRI CHA UPANDIKIZAJI FIGO AFRIKA

BMH , UDOM  na TOKUSHUKAI JAPAN WASAINI MAKUBALIANO YA KUANZA UJENZI WA KITUO CHA UMAHIRI CHA UPANDIKIZAJI FIGO AFRIKA

Published on May 26, 2025

Article cover image

Osaka, Japan 26/05/2025.

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) , Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) na Shirika la TOKUSHUKAI la nchini Japan wametia saini makubaliano ya kuanza Ujenzi wa kituo cha umahiri cha Upandikizaji wa Figo katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara-Afrika kinachotegemewa kugharimu Yen 1.5 billion sawa na TZS Billion 28. 

Makubaliano hayo yamesainiwa leo tarehe 26/05/2025 nchini Japan katika Osaka EXPO 2025 ambapo Mhe Kassimu Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa mgeni Rasmi.  Aidha, Watendaji wa taasisi hizo, Prof Abel Makubi wa BMH , Prof Lughano Kusiluka wa UDOM na Dr Shinishi, Mwenyekiti wa TOKUSHUKAI walishiriki kati kutia saini makubaliano hayo mjini Osaka. 

Kujengwa kwa kituo hicho cha Upandikizaji wa Figo, kutasaidia kuokoa maisha ya Wananchi wengi wenye uhitaji wa tatizo hilo .  Aidha , ushirikiano wa UDOM na BMH kwa pamoja , utawezesha kufanyika mafunzo na tafiti kuhusu umahiri wa kupandikiza figo  kwa watalaamu kutoka nchi mbalimbali za Afrika.