BMH YASHINDA TUZO YA KITAIFA KWA UBORA KATIKA UTOAJI NA MABORESHO YA HUDUMA

Published: Sep 29, 2026
BMH YASHINDA TUZO YA KITAIFA KWA UBORA KATIKA UTOAJI NA MABORESHO YA HUDUMA cover image

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imeibuka mshindi wa tatu kitaifa katika Kundi la Utoaji Bora wa Huduma na Maboresho, miongoni mwa taasisi na mashirika 308 ya umma yaliyotathminiwa na Msajili wa Hazina.

Tuzo hiyo imetolewa jijini Arusha na Mheshimiwa Deo Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa kikao cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi hizo.

Utambuzi huu unaakisi dhamira endelevu ya BMH katika kuimarisha ubora, ubunifu na utoaji wa huduma za afya zenye viwango vya juu zinazomlenga mgonjwa.