BMH YAPOKEA GARI NYINGINE YA KUBEBEA WAGONJWA
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imepokea gari nyingine ya kubebea wagonjwa hivyo kufikisha magari hayo matatu.
Akiongea wakati wa kukabidhi gari hiyo, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, (Mbunge wa Dodoma Mjini) amesema gari hiyo itasaidia sana kuboresha huduma za Hospitali.
"Nimshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuboresha huduma za afya," amesema Mhe. Mbunge.
Ndg. Mavunde ametumia fursa hiyo kuipongeza Hospitali kwa huduma nzuri inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dkt Alphonce Chandika.
"Hospitali hii inahudumia si wananchi wa Dodoma bali watanzania wote na tunapokea sifa nyingi kuhusu huduma zenu,"
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dkt Alphonce Chandika, anasema gari hii mpya ya wagonjwa inaweza kuhimili 'rough road' hivyo kupanua wigo wa kuhudumia wananchi.
"Sasa tunaweza kuhudumia wananchi katika mazingira yoyote hivyo kupanua wigo wa kuhudumia," amesema.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma (RAS), Ndg Kaspar Muya, amesema gari hii wa wagonjwa ni mkombozi wa vifo vya mama na mtoto.
"Hii gari ya wagonjwa inagusa moja kwa moja wananchi," amesema RAS.