MUUGUZI WA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA AMEPENDEKEZWA KUWA MUUGUZI BORA WA MWAKA.
Kumpigia kura fuatisha kiunganishi huki; https://voting.ths.or.tz/?utm_source=chatgpt.com
Kumbuka muuguzi bora wa mwaka jana ametoka Hospitali ya Benjamin Mkapa
Mfahamu Sr. Tumaini Mtatuu kwa ufupi.
2021 - 2023 Amekuwa kiongozi wa Wodi zote Hospitali ya Benjamin Mkapa, katika uongozi wake amefanya mengi baadhi ni haya.
· Ameanzisha mfumo wa kidigitali wa utunzaji kumbukumbu za wauguzi
· Ameanzisha ukaguzi na ushindani wa Idara za wodini na Kliniki ili kuleta ubora wa utoaji huduma za uuguzi
· Amewezesha kusimamia miongozo mbalimbali ya utoaji huduma ya wizara ya Afya ndani ya Hospitali
· Ameanzisha masanduku ya maoni wodini ili kuwapa fursa wagonjwa kutoa maoni juu ya huduma wanazozipata.
Kumbuka haya ni baadhi ya mambo aliyo yafanya