DKT MAGHEMBE: JENGEENI UWEZO HOSPITALII ZA CHINI LAKINI WASICHELEWESHE RUFAA.

Published: Sep 15, 2025
DKT MAGHEMBE: JENGEENI UWEZO HOSPITALII ZA CHINI LAKINI WASICHELEWESHE RUFAA. cover image

Na Ludovick kazoka na Jeremia Mwakyoma, Dodoma - Agosti 21, 2025

Hospitali ya Benjamin mkapa imetakiwa kuwajengea uwezo Hospitali za chini katika mikoa huku nao Waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa ya jirani na Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa wakielekezwa kuepuka kuchelewesha rufaa katika Hospitali hiyo ili kuokoa maisha ya Wagonjwa wanaohitaji huduma za Afya za rufaa.

Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt Grace Maghembe leo katika mkutano wa Kikanda wa uboreshaji huduma za Afya uliohudhuriwa na Waganga Wakuu wa Mikoa, Waganga  Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za  Mikoa na uongozi wa BMH.

"Sisi kipaumbele chetu ni usalama wa wagonjwa hivyo tuwaishe rufaa kwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa,"   amesema Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt Maghembe, wakati akifungua kikao hicho.


Dkt. Maghembe pia ameelekeza kuboreshwa kwa mawasiliano baina ya Hospitali za Rufaa za Mikoa na BMH kama moja ya njia muhimu ya  kuimarisha mfumo huo wa rufaa.

"Lazima tujengeane uwezo wa watalaamu wetu na tuboreshe mawasiliano ili kuimarisha rufaa kumuhakikishia huduma bora mwananchi na kuhakikisha mahitaji yote ya muhimu yanaandaliwa kuwezesha mgonjwa atakayepokelewa kwa rufaa anapata huduma inayostahili,"  Dkt Maghembe.

Dkt. Maghembe ameeleza Nchi inapoelekea kutekeleza Bima ya Afya kwa wote wananchi wanaangalia uwezekano wa kuzifikia huduma, kuzimudu na ubora.

"Mimi nimefika tu hapo getini nimepokelewa, naulizwa unaenda kwenye mkutano, wamenipokea, that's customer care," amesema Dkt Maghembe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof Abel Makubi, amesema BMH inapoelekea kuwa Hospitali ya Taifa ni muhimu kuimarisha mahusiano kati yake na Hospitali za Mikoa.

"Tunapoelekea kuwa Hospitali ya Taifa tuliona ni muhimu tukajumuika na wenzetu wa Mikoa inayotuzunguka ili kuimarisha mfumo wa rufaa na kuwaboreshea Wananchi huduma," amesema Prof Makubi.