EMBASSY OF TANZANIA, THE HAGUE

Published: Aug 26, 2026
EMBASSY OF TANZANIA, THE HAGUE cover image

UBALOZI WA TANZANIA, THE HAGUE

Leo Tarehe 24 Agosti, 2026 Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Netherlands umeupokea na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) @bmhdodoma , unaoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Prof. Abel Makubi, uliowasili nchini Netherlands kwa ziara ya kikazi inayolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya.

 

Ujumbe huo ulipokelewa na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi Bw. Charles Mmbando .

 

Mazungumzo hayo yalijadili kwa kina ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Netherlands katika sekta ya afya, na fursa zilizopo za kuimarisha na kupanua ushirikiano huo hususan katika maeneo ya huduma za kibingwa, mafunzo ya wataalamu wa afya, tafiti, ubadilishanaji wa uzoefu, teknolojia, ubunifu katika huduma za afya, pamoja na kujenga ushirikiano wa muda mrefu kati ya taasisi za afya za Tanzania na Netherlands.

 

Katika ziara hiyo, Ujumbe wa BMH unatarajiwa kufanya vikao na kutembelea taasisi mbalimbali za afya na taaluma nchini Netherlands zikiwemo Radbound Univerisity Medical Centre, ZGT-Overzee Foundation na SOTAC Convoy, kwa lengo la kujenga na kuimarisha ushirikiano kati yake na taasisi hizo na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano yenye manufaa kwa pande zote.

 

Kufanyika kwa ziara hii ni kielelezo cha jitihada za Ubalozi wa Tanzania Nchini Netherlands za kuunganisha Taasisi za Tanzania na Taasisi za nchini Netherlands ili kushirikiana katika kuimarisha huduma za afya, kujenga uwezo wa wataalamu, kubadilishana uzoefu na kuendeleza utafiti na ubunifu katika sekta ya afya.