HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA NI YA KISASA NA INAYOJALI WAGONJWA
HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA NI YA KISASA NA INAYOJALI WAGONJWA

Na Jeremiah Gasper Mbwambo, Dodoma, 23 Juni 2024.

Hayo yamesemwa na Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea banda la Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) katika kilele cha wiki ya utumishi wa Umma jijini Dodoma.

"Nawapongeza kwa huduma mnazozitoa ni za kisasa na zinazingatia utu, hatujasikia unyanyasaji wala vitendo vya rushwa kwa kweli tunawapongeza sana endeleeni kufanya kazi" alisema Mhe. Majaliwa

Kwa upande wake Bi. Prisca Lwangili Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu akimkaribisha Waziri Mkuu ameeleza namna BMH  ilivyo toa Huduma na Kutoa elimu kwa wananchi kupitia maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma.

"Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunayofuraha kwa kututembelea katika banda letu pamoja na huduma zinazotolewa hapa na BMH tumeendelea kutoa elimu juu ya huduma ambazo Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na matibabu ya Sickle Cell, matibabu ya figo ambayo tunapandikiza figo, matibabu ya moyo,  saratani, aidha tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa kwa Serikali chini ya Mheshimiwa Dr Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za kuanzisha jengo la matibabu ya saratani na huduma za upandizaji uloto ambazo ni za  kitaifa na kimataifa " Alisema Bi. Lwangili

BMH imekuwa ikitumia maonesho kama sehemu ya kusogeza huduma zake kwenye Jamii ya watanzania.

Dondoo za Afya na Habari
Kula Mlo Kamili
Kula Mlo Kamili

Eat a combination of different foods, including fruit, vegetables, legumes, nuts and whole grains. A...

  View more
Usivute Sigara
Usivute Sigara

Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mapafu yako, uvutaji wa sigara unaweza sababisha matatizo ya...

  View more
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta

Fats consumed should be less than 30% of your total energy intake. This will help prevent unhealthy...

  View more
Kuendesha Gari.
Kuendesha Gari.

Unashauriwa kutokuendesha gari kila siku na wakati mwingine unatakiwa kutembea walau miguu yako na m...

  View more
Epuka ulevi wa Pombe
Epuka ulevi wa Pombe

There is no safe level for drinking alcohol. Consuming alcohol can lead to health problems such...

  View more