TUZINGATIE UBORA WA HUDUMA KWA WANANCHI
Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka watumishi wa wizara hiyo kuongeza ubora wa utoaji huduma kwa kuwa afya si gharama bali afya ni uwekezaji wa kimkakati katika utu wa Mtanzania, uzalishaji wa uchumi, usalama wa taifa, na heshima ya nchi yetu.
Waziri Mchengerwa amesema hayo leo January 14, 2026 kwenye kikao kikao kazi na watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya na watumishi wa sekta ya afya na mkoa wa Dodoma katika Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa.
"Quality sio sehemu ya mfumo wa afya bali quality ndio mfumo wenyewe wa afya, katika huduma za afya hakuna nafasi za makadirio, hakuna nafasi ya kubahatisha, hakuna nafasi ya kesema tumefanya kadri ya uwezo wetu bali kila hatua inaathari ya moja kwa moja kwa mwanadamu," amesema Waziri Mchengerwa