TUPUNGUZE MUDA WA MGONJWA KUSUBIRIA KUPATA HUDUMA ILI MTEJA APATE HUDUMA KWA WAKATI
Na Ludovick Kazoka na Gladys Lukindo: Dodoma Feb 25
Muda wa mgonjwa kusubiria kupata huduma (Turnaround time) unapaswa kupunguzwa ili mteja apate huduma kwa wakati.
Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Prof Abel Makubi, akisema kuwa vipimo na matibabu vitolewe kwa wakati.
"Mgonjwa apate huduma za vipimo na matibabu kwa wakati," amesema Mkurugenzi Mtendaji wa BMH wakati wa programu ya CME.
Programu ya CME leo Jumatano imeangazia umuhimu tiba bobezi za radiolojia (interventional Radiology)
Mkuu wa Idara ya Interventional Radiology, Daktari bingwa wa interventional Radiology, Hasna Nuhu, ameelezea umuhimu wa huduma hii mpya ya radiolojia kwa idara zote hospitalini.
"Interventional Radiology ni mtambuka kwa maana ya kuhusika katika kila idara ya hospitali," amesema Dk. Hasna.
Aidha, Daktari Bingwa wa Interventional Radiology, Furaha Malecela, amesema kuwa tiba bobezi za radiolojia ni mtambuka kwa huduma zote bobezi, hivyo kutoa mchango mkubwa katika matibabu.